0 0
Read Time:1 Minute, 24 Second

WU®Media PRODUCTION

DODOMA: 1/04/2022

Chama Cha Mapinduzi CCM kimefanya Mkutano Mkuu maalumu uliofanyika Leo tarehe 1/04/2022 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete. Katika mkutano huo Pamoja na kufanyia marekebisho vifungu kadhaa vya katiba ya Chama lakini pia alichaguliwa Comrade Abdulrahman Kinana kuwa makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM taifa Tanzania bara. Uchaguzi huo umefanyika baada ya Comred Philip Mangula kung’atuka. Ndugu Kinana alichaguliwa kwa kura zote za ndio.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Wazee nchini kwa kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wa kuleta maendeleo nchini kabla ya kufunga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akiondoka katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma.
 
Viongozi mbalimbali wa Chama pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupitisha marekebisho ya Katiba ya Chama ya mwaka 1977 pamoja kumpigia kura kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana leo tarehe 01 Aprili, 2022.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, Wanachama pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wakati akifunga Mkutano huo Maalum uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %