0 0
Read Time:3 Minute, 3 Second

WU®Media PRODUCTION LIMITED

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
April 6,2022.

Hakuna wakati nzuri ambao vyombo vyetu vya Habari Nchini vingeutumia kuisaidia Serikali ya AWAMU ya SITA kupiga hatua ZAIDI za kimaendeleo, kama wakati huu wa Mh. Rais wangu,Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye ameonekana ni wazi kuwa muumini mzuri wa uhuru wa watu kusema”One Nation One Common Vision”.

Majuzi Mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan, amenukuliwa akiwaambia wadau wa siasa na wadau wa maendeleo kuwa, Nchi hii ni yetu yote hivyo wote tunawajibu wa kuijenga kwa kuchangia mawazo no matter upo upande gani wa siasa za NDANI ya Nchi!A very big wakeup call kwa watu wanajua wajibu wao kwa Taifa lao!

Wakati Ndugu yangu Balile na wanahariri wenzake walipokaribishwa ikulu na Mh.Rais Samia alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari,moja ya hoja waliyoibua ilikuwa uhuru wa vyombo vya habari na biashara ya vyombo vya habari!Ni kama Mr Rais kashafanyia kazi ombi lao maana mpaka Kaka yangu Said Kubenea na magazeti yake”Mwanahalisi” yaliyopotea pia nae amefunguliwa!

HOJA ZANGU HIZI HAPA!

I.Ni kama media ya Tanzania kwa sasa imeshindwa kuisaidia Serikali ya AWAMU ya SITA kupiga hatua za haraka!Mfano nilitegemea KAULI ya Mh.Rais kwamba Nchi imerudi tena kwenye nafasi yetu ya awali ya LDC’s ingekuja na stories nyingi sana!Nini kimetokea?lakini “sisi” tumeachia social media zetu ambazo hazina hata “gate keepers”ndio zitawale mijadala?

Kuziruhusu social media ndio ziwe drivers wa kubua na kutuendeshea mijadala mikubwa yenye maslahi mapana kwa Nchi ni HATARI sana!Huu mjadala wa Tanzania kurudi kwenye kundi la LDC’s, bila ujasiri wa Mama YANGU Samia wengi tusingejua!Mchumi Zitto Kabwe nae kimya!Unashangaa!

II.Rais wa SMZ Hussein Mwinyi aliwahi Kusema”….bora mtu anikosoe nijue ninapokosea….kuliko kunisifia tu,sababu mwisho wa siku kuna KITU unakitaka..ndio maana unasifiwa…..”

Ni wazi kuwa Serikali ya AWAMU ya SITA imefanya makubwa NDANI ya mwaka mmoja lakini bahati mbaya media ya Tanzania pia imekuwa kama sehemu ya sisi wanasiasa kwa kusifia bila kusema kwamba tungeweza kufanya makubwa ZAIDI ya haya”watch dog role & responsible media”.Nilitegemea kaka YANGU Machumu wa pale MCL angekuja na analysis ya kuisaidia Serikali tunarudije kwenye status yetu awali ya Uchumi wa kati?,Nini kimetokea?,kaka zangu Machumu na Mwigamba pamoja na kuwa na watu weledi ndani ya newsroom zao bado hajatuambia!Wapo kimyaaa!

III.Mpaka sasa sioni balance nzuri ya uwepo ya uwingi wa vyombo vya Habari,kuongezeka kwa uhuru wa habari dhidi ya uwepo wa responsible media na development journalism!Rais wangu na Mama YANGU,Mh Samia aliwahi kusema”…uhuru tunaoafuta lazima uendane na wajibu wetu kwa Nchi yetu!

IV.Kwa maoni yangu,uhuru huu ambao tulikuwa tunautafuta wakati wa AWAMU ya tano na “kuukosa” na tukaupata kupitia Serikali ya AWAMU ya SITA,utakuwa hauna maana kabisa kama media itaendelea kwa “toothless dog” kama sasa!

Ile dhana ya Media as a Fourth Estate imekufa kifo kibaya wakati huu ambapo hakuna kabisa “the culture of intimidation & suppression”!Nauliza nini hasa kinatokea katika Tanzania yangu?

V.Lazima Chama changu yaani CCM kikubari kuwa ni hatari mno kuendelea kupigiwa makofi na media wakati huu kuliko tulivyokuwa tunasutwa awamu ya tano!Infact hatupo salama sana wakati huu sababu tunakosa kioo cha kutuambia tumechafuka au laa!Wakati bunge letu lina zaidi ya wabunge asilimia 90 wa CCM lakini kibaya zaidi tumekuwa na “toothless dog”!

Tumekuwa na kioo ambacho kila siku kinatuambia”jamani” mmependeza na kama wanatuambia ukweli,basi tunapiga hatua nzuri ZAIDI!

Kama huu ndio uhuru ambao professionals wenzangu walikuwa wanautaka basi ni bora kaka YANGU Said kubenea arudi kwenye lockup yake ya awali!Gharama ya VYOMBO vya Habari huru haiwezi ikawa ni hii ya sasa!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %