0 0
Read Time:5 Minute, 27 Second
Jicho la Uledi

WU® Media PRODUCTION LIMITED

CCM YA ABDALLAH BULEMBO VS CCM YA LUHAGA MPINA!

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
April 8,2022.

CCM ya ndugu yangu na Mzee wangu,Mh. Abdallah Bulembo, Mwenyekiti wetu wa zamani wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, inaweza kufa haraka zaidi dhidi ya CCM ya Mh. Luhaga MPINA!Katika dhama hizi mpya bado NDUGU Abdallah Mulembo anaogelea kwenye bwawa la “The culture of silencing”.

Kuna msemo unasema,Nanukuu kidogo”…absolute power may collapse absolutely…”

Chama dola kikubwa kama CCM kwa nyakati hizi za sasa,endapo kikiruhusu maoni hafifu ya watu hafifu kama Mzee wetu, ndugu Abdallah Bulembo,kitakufa!”State failure”!

Wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika HIVI karibuni Jiji Dodoma,pamoja na mambo mengine,kumpitisha Makamu Mwenyekiti wetu mpya wa CCM Taifa,Mzee wetu Afande Kanali(rtd) Abduhaman Kinana,Mzee huyu alisema,Nanukuu;

“…Nina mambo makubwa matatu ntaenda kuyafanya …lakini kubwa zaidi ni kukuza demokrasia ndani ya Chama …”!

Pamoja na mambo yote yaliyosemwa KUHUSU Afande wangu Abdahman Kinana, baada ya uteuzi na kuthibitishwa kwake ndani ya chama lakini bado kwangu Mimi,Mzee Kinana anabaki kuwa only & political strategist muhimu sana ndani ya wakati huu na ndani ya CCM!Kwa upepo huu,CCM yangu ya sasa, ilimuhitaji mno au inawahitaji mno watu kama Mzee wetu Kinana kuliko watu dhaifu kama akina Mzee wangu Abdallah Mulembo!

Ni wazi kuwa kwa sasa,CCM ya Mama Samia Suluhu Hassan, inaendelea na itaendelea kupambana na kukumbana na mashinikizo mengi zaidi ya yale jana,na hii ni kwa sababu ya misimamo wa Mh. Rais JMT na Mwenyekiti wa CCM Taifa,Mama Samia Suluhu hassan!“Fair Fair Policy”

Rais wangu wa sasa Mh.Mama yangu Samia Suluhu Hassan,anaonekana kuwa ni muumini mzuri wa kukosolewa na anahitaji sana kupata mawazo nje ya CCM yake Ili kuweza kuendesha NCHI vizuri kabisa!Kwa kujua hilo,technician Afande Kanali(rtd) Abdulaman Kinana baada ya kupewa NAFASI ya kuongea pale Dodoma akatembea mulemule kwenye ubongo wa Mama Samia”opinion diversity within a Party”.

Hapo ndio unaweza kuona tofauti kubwa na akili kubwa ya afande Kanali wa Jeshi Abdahman Kinani dhidi ya akili ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM miaka hiyo yaani Mzee wangu Abdallah Bulembo!”Political strategism gap”.

Maadui wetu wa ndani na nje ya chama, kwa sasa tunaweza kuwazuia kwa strategia na sio kwa hisia tu!Kaka yangu Hamfrey PolePole nadhani huko aliko anacheka,hii ndio CCM bwana!Matamko ya watu kama Mzee wangu Abdallah Bulembo yanatupunguzia uhalali sana MBELE ya WATANZANIA na kama Mzee huyu anadhani anailinda CCM ya sasa bado nataka kumwambia kuwa, anatupoteza zaidi!

Mwalimu Julias Kambarage Nyerere aliwahi kusema na hapa nanukuu,”…Chama legelega uzaa Serikali legelege…”

Watu kama Mh.Luhaha Mpina wanatusaidia sana kujenga Serikali imara ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu ambao kwa vyovyote unaweza kuwa mgumu sana kwetu japo kushinda ni lazima!Tuwaze pamoja!

UKWELI WA SIASA ZA TANZANIA KWA SASA!

I.Mpaka sasa TAARIFA za ndani ya CDM zinasema kuwa,mpaka sasa CDM wana target ya majimbo “yao 45” ambayo wenyewe wanasema wana uhakika kabisa wa kushinda na CDM, wameshaanza kuchora ramani zao kimya kimya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025!

Nenda pale wilayani Ikungi kwa kaka yangu,cde Jerry Murro,kuna kibanda cha Mzee mmoja”fundi Cherehani”kinagawa hotuba za Tundu Lissu kama njugu usiku wa manane!Mzee Abdallah Bulembo anapaswa atusaidie sana jinsi gani tutawazuia CDM na mpango wao wa majimbo 45!Huu ndio msaada muhimu ndani ya CCM kwa sasa!

II.Ni wazi kuwa mpango wowote wa kuwanyamazisha watu wenye kutushauri vizuri zaidi ndani ya CCM unaweza kuzaa upinzani mwingine mkubwa ndani ya CCM yenyewe na nje ya CCM pia!Tukubaliane kuwa watu kama Luhaga MPINA ni wengi mno ndani ya CCM kwa sasa na njia bora ya kideal nao ni kuwapa NAFASI ya kusema,kusema na kusema!Kuanza kupambana nao kwa sasa ni kujipotezea uhalali hasa wakati huu ambao watu hawa(Mpina,Abbod na wenzake” wamekuwa wakisimama na kutembea kwenye hoja nzito na hoja za msingi zenye maslahi mapana ya CCM na maslahi ya Taifa!

III.Nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu kwa CCM ya Samia ni kubwa zaidi ya jana lakini USHINDI huo utategea sana jinsi gani CCM inaweza kuassemble “vichwa “muhimu ndani ya Chama husika na kuvitumia vizuri zaidi!

USHINDI wetu wa uchaguzi wa mwaka 2025, utategemea sana na jinsi gani Chama na Serikali ya CCM,inavyoweza kuchukua hatua dhidi ya WATUMISHI WA Serikali Kama cde Makamba ambao ni wazi wameshindwa kutimiza wajibu wao na sio kutumia nguvu kubwa isiyo na tija kuwazuia watu kama Mh. Luhaga MPINA!Najua tunajua kuwa, kwa sasa tuna wakina Luhaga Mpina wengi ndani ya Serikali na ndani ya Chama!Tunajua!

IV.CCM tunapaswa kujua kuwa kifo cha hayati John Pombe Magufuli kimebadili mno siasa zetu za ndani ya CCM na nje ya CCM,lazima tukubali hilo!Kama huo ndio ukweli wenyewe,CCM yangu inapaswa kuwa makini sana wakati huu kuliko wakati wowote ule!

Public opinions zinaonyesha wazi kuwa kuna “public dillema” kubwa sana kwa sasa na wapinzani wetu obviously watataka kuitumia hiyo vaccum!What do we do kama Chama?

Tumwachie Afande Kinana kwa Sasa!Kazi hii aliwahi kuifanya vizuri mwaka 2014 pale CCM ilipokuwa imepoteza mvuto sana kwa wananchi”public dillema”lakini Mzee wetu afande Kinana na timu yake wakaweza kutupa USHINDI,akatuvusha salama!

V.Watu kama Luhaga MPINA(Mb)wanapaswa kujibiwa kwa hoja nzito zaidi na vijana wa CCM na vijana smart waliopo serikalini, uwezo kwa kujibu hoja hizo tunao!Hakuna haja ya kupanic!Uwezo wa “kumaneuver”hoja za Luhaga Mpina upo ndani ya vijana wa CCM lakini bahati mbaya hatupewi hizo NAFASI za kujibu mapigo!

Nilisema hapo juu kuwa moja ya failure yetu kubwa ndani ya CCM ni kukosa uwezo wa kutambua uwezo wa watu na vijana wake ambao labda wangeweza kukusaidia Chama wakati huu!Nilitegemea Kijana wa CCM atoke na hoja nzito zaidi za kuisemea Serikali na sio hoja nzito za kuzuia Serikali ya CCM isisemwe!

Watu kama Luhaga MPINA wana hoja nzito na kamwe tusiwajibu kwa hoja dhaifu!Sisi ni Chama tawala chenye hazina ya vijana wasomi na wenye kujua na uwezo wa kucheza na “wakina Mpina” ambao ni wazi wapo wengi ndani ya Serikali na ndani ya Chama changu kwa sasa!

CCM inahitaji sana kusoma uwanja wa medani wa siasa za sasa ndani ya CCM na nje ya CCM kwa sasa kabla ya kuanza kumshambulia adui!Mwacheni kamanda Abduhaman Kinana achore ramani vita ya CCM kuelekea 2025.CCM mpya ya Kanali Kinana ina uwezo mkubwa wa kumpiga adui majini,angani na aridhini!Mzee wangu Abdallah anapaswa kukaa kimya!Waache waje!

+255784159968

WU®Media PRODUCTION LIMITED

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %