
WU® Media PRODUCTION LIMITED
Ubalozi wa Tanzania Sweden umewakutanisha Diaspora kwa futari iliyoandaliwa na Balozi wa Tanzania Sweden Mh Grace Olotu. Wadau wamemshukuru Sana Balozi kwa maandalizi mazuri na kuwakutanisha Watanzania wote katika mwezi mtukufu wa Ramadhan..
“Tunatoa Shukran za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kwa kutoa Sadaka ya Futari kwa Diaspora wote.Pia tunawashukuru Diaspora wote walioweza kufika na kushiriki Futari ya pamoja .Asanteni sana kwa kuonyesha upendo na mshikamano.” Jason Junior.















