
WU® Media PRODUCTION LIMITED
KWANINI MH JOB AGUSTINO NGUGAI AMEPOKELEWA KWA SHANGWE BUNGENI?

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
April 14,2022.
Ni wazi kuwa Bunge la Dr.Tulia Ackson Mwansasu la kuanzia mwaka 2020 mpaka mwaka 2025 linaweza kuisumbua sana Serikali ya CCM kuliko mabunge yote yaliyowahi kutokea katika siasa za vyama vingi Nchini!Dalili zi wazi sana kupitia maelezo!
Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linataka kujificha kwenye dhana ya wajibu wa Bunge na mbunge mwenyewe wa kuisimamia Serikali”check & balance” huku wakiachana na dhana ya collective responsibility ambayo ndio dhana Bunge la mwaka 2015 mpaka 2020 iliisimamia!
Dalili zi wazi kabisa kuwa Bunge la Dr Spika Tulia Ackson japo linaundwa na wabunge zaidi ya asilimia 95 wa CCM lakini linaonekana mapema kabisa kuwa linaenda kuizofisha Serikali ya CCM kuliko kuijenga!CCM inapaswa kuwa macho zaidi na Bunge lake lenyewe zaidi ya kuigopa CDM!
Kuna umuhimu chama changu na serikali yangu ya CCM wafanye haraka kujua nini kinaendelea na nini kitakuja!Sio kawaida sana katika Serikali iliyopita,kuona mawaziri wa CCM wanazodolewa waziwazi na wabunge wenzao wa CCM kweupee!
Eti leo hii, Bunge hili linakuwa “nzito” kwa Serikali ya CCM zaidi ya Bunge la John Mnyika,Godbless Lema, Peter Msingwa, Mr II Sugu na Freeman Mbowe!
Swali langu hapa je,ni nia njema na uhuru wa Bunge au ni usaliti yaani kama “bwai na iwe bwai?”.Lkn je,kama bwai hii inatokana na nini?kelele zote HIZO Dodoma za nini?
“…Serikali itueleze SABABU za kupanda kwa gharama za maisha na waje na majibu ya jinsi ya kuwaokoa wananchi…”.
“…..naomba kuliomba Bunge lisitishe shughuli zake kuweza kujadili hali ya kupanda kwa gharama za maisha Nchini….”
“…kwanini Serikali haitaki kuweka ghala la mafuta …ili wakati huu wa matatizo tunafungulia mafuta yetuuuu…..?”.
Utadhani Mbunge huyu Mh.Kibajaji hajui kuwa tuna Tipper pale Kigamboni Dar es salaam!Utadhani Serikali zote huko nyuma zilijenga maghala ya mafuta halafu akaja Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akayabomoa!
KWANINI BUNGE HILI LINAWEZA KUIBOMOA AU KUIJENGA SERIKALI YA CCM KWA SASA?
I.Hakika kama Mh. Spika Mstaafu Job Austino Ndugai alikuwa anaumwa ugonjwa wa malaria nadhani jana atakuwa amepona kabisa kwa sababu kishindo kile kikubwa ndani ya bungeni kingetosha kumtibu malaria yake!sijui kama naeleweka vizuri!
Kuna tafsiri kubwa mbili hapa kuhusu makofi yale ya dakika tano pale Bungeni, baada ya Mh.Ndugai Job kutambulishwa kwake(I)Moja,Job Ndugai basi alikuwa anakubalika sana ndani ya Bunge la 2020/25 la CCM lakini pia yaweza kuwa (II)makofi yale yalimaanisha kumcheka baada ya kupoteza kiti chake “kibingwa”.Za kuambiwa,changanya na zako!
II.Uwepo wa mashambulizi ya waziwazi kutoka kwa wabunge wa CCM kwenda kwa baadhi ya mawaziri hasa Waziri mwenye dhamana ya Mafuta na Bwawa la Umeme la Rufiji kunatia shaka sana!Pima uone mwenyewe!
Mimi kijana wa CCM sometimes nakaa weeee na unajiuliza,je,ile dhana ya Serikali ya CCM ya awamu ya tano ya kusimama kwenye “collective responsibility”imefia awamu ya sita?kwanini ifie awamu hii?!Wakuu wangu wa CCM lazima tukae chini tuone na kama kuna nongwa sehemu tuyaweke sawa mapema kabisa kabla haijawa noma!
Alianza kaka yangu Luhaga Mpina kulia na Waziri wa Nishati,January Makamba,akaja Shabiby akalia na Makamba,akaja Livingstone Lusinde akalia na January Makamba na pia akaja Mh.Tabasamu akalia na January Makamba!Wote hawa walikuwa wagumu angalau hata kupepesa macho, yaani ilikuwa “”show show”!
III.Maana zima ya kulilia “Bunge live” kweli imepata mashiko makubwa kwani wabunge wa CCM kwa sasa ni kama wanataka kujiuza”wenyewe” badala ya kuiuza CCM na serikali ya awamu ya sita!
Umemsikia Askofu na Mzee wangu Dr. Gwajima?Ni kama anasema Nchi yangu Tanzania haina maono kwa sasa ya pamoja na bahati mbaya sana, wabunge wa CCM ndio wanaongoza kwa kupiga makofi kukubali kuwa Nchi eti haina maono kwa sasa!Duuu!
Yaani Askofu Gwajima anataka kusema Serikali ya awamu ya tano ilikuwa na maono ya kitaifa”common vision & direction” lakini Serikali hii ya awamu ya sita haina maono yoyote na wanaccm wenzangu na CCM kama Chama tumekaa kimyaaa!jamani!Huyu Mzee wangu Askofu Gwajima hata hatujamalizana nae Ishu ya kwanza anakuja tena!Lkn pia huyu ndio yule aliyechukua nafasi ya “Anko Furaha pale Kawe,kasahau ghafla?
IV.Leo Mh Halima Mdee kutoka CDM alipokuwa anamwaga hoja nzito za “kuizodoa” Serikali ya CCM kuhusu eti kushindwa kwake kuendesha Shirika letu la Ndege na akawa anataka kupinga mpango wa Serikali ya CCM wa kuongeza Ndege sita mpya, hakuna hata Mbunge mmoja aliyesimama kuweka rekodi sawa zaidi ya watu wawili tu yaani mjumbe mmoja wa kamati ya miundombinu na Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba!
Nikawa najiuliza hii ndio CCM ya wapi hii?wabunge wa CCM zaidi ya 300+ leo wanashindwa hata “kugoggle” haraka haraka na kuchallange taarifa za Mh.Halima Mdee?Binti alipoona tumelala,akamua kutuchamba hatari!
V.Hivi hii dhana ya kwamba baadhi ya wabunge wetu kuhisi hawapo salama kuelekea mwaka wa uchaguzi na uteuzi 2025 nani anawadanganga?!Nani kakwambia kuwa hauna nafasi 2025 kiasi kwamba mpaka mmeamua kuwa mabubu na kutokukisemea Chama?Ni wazi kuwa uteuzi wa Mbunge wa CCM utategemea mambo haya ya msingi!
(I)ushiriki wako kwa wananchi wako katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kuleta maendeleo katika eneo lako kwa maana ya Jimbo lako(II)Utii wako kwa Chama na serikali ya chama cha mapinduzi na (III)juhudi zako binafsi nje ya utaratibu wa Chama katika kuwaletea watu wako maendeleo!
Hakuna mwenye muamala na CCM ya MhSamia Suluhu Hassan,ukiambatana na sisi leo na sisi tutaambatana na wewe kesho!HIYO ndio “Slogan Yetu”.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kazi Iendeleee!
+255746726484








