0 0
Read Time:1 Minute, 21 Second

WU®Media PRODUCTION LIMITED

Waandishi Mashuhuri Duniani “Kucover” Uzinduzi “Tanzania; the Royal Tour”

Na Mwandishi Wetu, Diaspora News, NY

Achana na orodha ya kihistoria ya waalikwa ambayo itakuonesha nguvu na uwezo wa kisiasa wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, hapa tunakuletea baadhi ya wanahabari mashuhuri duniani na vyombo vyao walioalikwa kuandika tukio hili leo hapa New York.

Nimeona katika mialiko atakuwepo Sandra Gonzalez wa CNN lakini kutoka Hollywood Life mwandishi Bonnie Fuller naye atakuwepo. Lakini ukanda wa magharibi mwa Marekani (West Coast) bado utawakilishwa tena na Ashley Lee wa Los Angeles Times.

Waandishi ni wengi na jambo hili halijavuta tu usuasi mkubwa huko nyumbani pia diaspora wa hapa lakini niseme tu ni watu wa nchi nyingi kwamba watakuwepo pia wanahabari kutoka New York Times, Entertainment to Night, Vanity magazine, CBS, majarida mashuhuri kama Vogue, Essence na mashirika mashuhuri ya habari mengine kama Bloomberg, Fox News na Huffington Post na The Hollywood Reporter.

“Kuna matukio mengi leo siku yenyewe ya uzinduzi wa kwanza hapa New York ikiwemo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na watu mashuhuri wa hapa katika sekta mbalimbali za biashara, burudani na habari akiwemo kiongozi mmoja mashuhuri wa New York, lakini sisi tuko hapa Guggenheim ukumbi utakapotumika na kila kitu kimekamilika,” ameeleza Dkt. Hassain Abbasi mmoja wa viongozi wanaoratibu Royal Tour.

Kwa hapa Marekani leo ni kituo kikubwa katika mfumo wa matangazo wa umma (pbs) cha wttw au chaneli 11 tu kitakachoruhusiwa kurushia filamu hiyo. Vituo zaidi ya 300 kisha vitafuata baada ya hapo na kisha itaoneshwa nje ya hapa Marekani na katika mitandao ya kijamii.

https://youtu.be/HES8WheVj4U

WABONGO UGHAIBUNI MEDIA PRODUCTION LIMITED

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %