
WU®Media PRODUCTION LIMITED
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Mabalozi wa Nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Mabalozi wa Nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya Futari aliyoiyandaa kwa ajili ya Mabalozi hao Jijini Washington Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan yupo Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo Pamoja shughuli zingine za kuipaisha Tanzania katika nyanja za kidiplomasia, kisiasa na kiuchumi pia atashiriki uzinduzi wa Film ya Royal Tour ambayo inakwenda kuitangaza nchi ya Tanzania Duniani kwenye sekta ya Utalii na uwekezaji. Safari za Mh Rais tangu aingie madarakani zimekuwa zikileta matokeo chanya kwa nchi na mara nyingi amekuwa akitoa mrejesh wa safari zake kwa Wananchi yeye mwenyewe kila anaporejea nchini.











