Na Mwandishi wetu
WU® Media PRODUCTION LIMITED
Josephine Favre President wa vertical farming anaeishi nchi Switzerland, amekutana na Balozi wa Tanzania Italy Mhe. Mahamoud Thabit Kombo na kufanya mazungumzo kuhusu changamoto anazopitia katika kutimiza Nia yake ya kutoa mafunzo ya kilimo kwa vijana na akina mama. Kilimo ni moja ya kipaumbele Cha mipango ya Maendeleo ya Tanzania,hivyo kunahitajika dhamira za makusudi katika kuongeza tija kwa Taifa na Maendeleo kwa jamii huku kukizingatiwa mazingira yenye usalama kwa chakula.
Madam Josephine favre alimueleza Mh Balozi kuwa Mkakati wa mafunzo ya muda mrefu kwa vijana zaidi ya 4000 wa Tanzania juu ya miundombinu ya Kilimo kuwa sio tu watatoa mafunzo kwa vijana wa Tanzania, bali pia utaongeza nafasi za kazi katika tasnia nzima ya kilimo.
Mh Balozi alimuhakikishia Josephine favre kutoka AFRICAN ASSOCIATION FOR VERTICAL FARMING yenye ofisi zake nchini Switzerland, ushirikiano na Serikali ili kuondoa mkwamo na kufanikisha mradi huo.
“Tanzania ni nchi yangu Mama na siwezi kujivunia zaidi ya kuchangia juhudi zangu katika ardhi ya mababu zangu” alisema Madam Josephine favre wakati akimshukuru Mh Balozi kwa kutenga muda wake,kukutana nae na kumsikiliza changamoto zake.
Katika Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati kuu ya Diaspora Italy Ndugu Ricky Johnson Bondo, Mh Balozi aliambatana na Bi Jacqueline Boniface Mbuya ambae ni ofisa wa Ubalozi na muwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika mashirika ya kimataifa FAO, IFAD & WFP mjini Rome Italy.
Akiongea na Wabongo Ughaibuni Media WU® kwa njia ya simu, President Josephine Favre alisema “Mkutano kuhusu elimu ya Kilimo kwa vijana wa Tanzania na Mheshimiwa Balozi Mohamud Thabit Kombo mjini Rome ulikwenda vizuri sana.”