Na Kagutta Maulidi
WU® Media PRODUCTION LIMITED
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mwenyekiti mpya wa Chama Cha ACT WAZALENDO kwa mara ya kwanza tangu KUCHAGULIWA.
Mkutano Mkuu maalum wa ACT Wazalendo, katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, umemchagua kwa kura nyingi Juma Duni Haji (Babu Duni), kuwa mwenyekiti wake mpya. Atakuwa mwenyekiti wa tatu wa chama.
Ndugu Juma Duni Haji, mara baada ya kuchaguliwa aliomba kukutana na Rais Mwinyi kwa Nia ya kujitambulisha na kupata fursa ya kuchomeka mawili matatu yanayohusu mustakabali mzima wa serikali ya umoja wa Kitaifa visiwani Zanzibar.
Rais Mwinyi amesema mazungumzo yao yamekwenda vizuri. RAIS Mwinyi amekuwa na usikivu Mkubwa kwa kila kada na hata mwananchi mmoja mmoja,huku akitanguliza maslahi mapana ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.