WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Mhe. Samuel William Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi jijini Paris France, ambaye pia ni Mwakilishi wa Tanzania kwenye UNWTO akishiriki Kikao cha Kwanza cha Dharura cha Baraza Kuu (First Extraordinary Session of the UNWTO General Assembly), Madrid-Uhispania tarehe 27.04.2022
Kupitia kikao hicho, Nchi Wanachama wa UNWTO wamepitisha Azimio la kuisimamisha uanachama Urusi kwenye Shirika hilo. Kama ilivyoainishwa kwenye sera ya mambo ya nje ya nchi, Tanzania ilipiga kura ya kutofungamana na upande wowote kwenye rasimu ya Azimio hilo.