0 0
Read Time:57 Second

WU® Media PRODUCTION LIMITED

Balozi wa Tanzania Nchini Italy Mheshimiwa Mahamoud Thabit Kombo ameongoza baadhi ya Watanzania katika tafrija fupi ya kukata keki ikiwa ni ishara ya kusheherekea Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa April 26, 1964

Balozi Kombo amesema Watanzania wanayokila sababu ya kujivunia juu ya uwepo wa Muungano huo ambao umekua chachu ya kuleta maendeleo na kuibua fursa mbalimbali.

Utangulizi huo wa ukataji wa keki utafuatiwa na sherehe maalumu ya kusherekea Muungano inayoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Roma. Sherehe itafanyika siku ya tarehe 7/05/2022 mjini Rome na inategemewa kuhudhuriwa na Diaspora nchini Italy kutoka maeneo mbalimbali. Kwa mujibu wa tangazo sherehe zitafanyika kwenye anuani hii VIA TUSCIA 95 ROME na Mgeni rasmi atakuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Italy ,Mh. Mahamoud Thabit Kombo.

Katika hafla hiyo,Mh Balozi alituma salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan za kumuunga mkono na pongezi kwa kuadhimisha Miaka 58 ya Muungano akiwa ni Rais awamu ya sita.

Sisi Ubalozi na kituo Cha Roma Tunakuunga mkono katika kusherekea miaka 58 ya Muungano wetu na Tunaomba upokee Salaam hizi”

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %