0 0
Read Time:2 Minute, 19 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Na Dr Yahya Msangi

TOGO West Africa

MIZENGWE YA WORLD CUP

Katika utumishi wangu nilibahatika kuwa mjumbe wa vikundi kazi (TASK FORCES) mbalimbali Kimataifa. Nazikumbuka 2 kwa leo na zoote hizi 2 zilihusu mpira wa miguu aka soka. Na zoote zilihusu Kombe la Dunia.
World cup ya Brazil (BRAZUCA)
na hii ya Qatar (AL RIHLA).

NCHi za magharibi huwa hazipendi Kombe la Dunia liandaliwe Nje ya NCHI Zao. Hufanya Kila jitihada kuzichafua Nchi zinazo “thubutu” kuandaa Kombe la Dunia.

Mwaka 1970 Mexico ilipoandaa zilizuka tuhuma kuwa héla ya unga imetumika kujenga viwanja. Ilipoonekana imebuma ikaambiwa “altitude” ya viwanja haswaa kile cha
“Estadio Azteca” ilipochezwa fainali ilipendelea timu za America Kusini! Brazil iliifunga Italy kwenye fainali. Mpaka Sasa imekuwa ngumu Mexico kuandaa world cup tena kwa kisingizio hiki.

Mwaka 2014 Brazil ilipopewa Fursa ikasemekana kiwanja kikuu cha Maracana kimepoteza hadhi ya kuandaa fainali. Brazil ikasema itakiboresha. Na ikaanza Kujenga viwanja vipya majimboni. Ikazuka hoja mpyaa kwamba katika ujenzi Kuna unyanyasaji wafanyakazi, malipo kiduchu na ubaguzi dhidi ya wahamiaji haramu na LGBTIs!

Basically Brazil ni nchi yenye wakatoliki wengi hivyo haya mambo ya haki wanazotetea kina Lissu wengi hawakubali. Hivi wakurya wakienda Kujenga kiwanja London na wakataka kichuri watawapa? Au wachaga waende Kujenga Italy watake Mbeke na ndizi utumbo watapata?

Hâta ya South Africa MIZENGWE ilikuwepo! Mara vuvuzela, mara corruption, mara low quality of service na viwanja, n k. Ni kuweka mazingira iwe ngumu tena kuandaa kombe Afrika!

Qatar ilipopata uandaaji kwanza ikasemekana wamehonga! Ushahidi ulipokosekana ikasemekana wananyanyasa wafanyakazi wahamiaji, hawaruhusu mashoga na wasagaji kujenga viwanja, wanasilimisha wafanyakazi kwa nguvu, hawaajiri wanawake, n.k.

Bahati nilikuwa miongoni mwa vikosi kazi vya kuchunguza tuhuma Brazil na Qatar. Mimi kitengo changu kilikuwa kuangalia tuhuma kuhusu masuala ya Ajira (employment – core ILO Labor Standards). Nyakati Hizo nilikuwa mratibu mkoa ( Régional Coordinator – International Trade Union Confederation) yenye makao makuu Bruxelles.

Kila kampeni Hizi zilikuwa na slogan yake. Mfano ya Qatar ikiitwa “NO WORLD CUP IN QATAR WITHOUT LABOR RIGHTS”!

Katika nchi zoote mbili kila mmoja wetu aligundua upotoshaji mkubwa uliokuwa ukifanywa na nchi za magharibi zikishirikiana na kina Oxfam, Human Rights Watch, UN HR Commission! Hâta baadhi ya watumishi wenzetu wakitumiwa kusambaza propoganda.

Kuna machache yalikuwa na ukweli LAKINI mengi yalitiwa chumvi kupita kiasi. Na mengine ni île tabia ya k8magharibi kutaka kulazimishia Mila, tamaduni na ubaradhuli wao kwa nchi za wenzao.

Kulikuwa na double standards! Hivi mbona Kombe la Dunia linapoandaliwa na nchi za magharibi hakuna tuhuma wala vikosi kazi kuchunguza?

BAADA ya TAARIFA zetu ilishindikana kuzipokonya Brazil na Qatar uandaaji. Sasa Qatar inawaonyesha wao iko héla! Inaandaa world cup ya miujiza! Itachukua miaka mingi kiwango cha Qatar kufikiwa hâta na wa magharibi! Qatar anataka kuwaonyesha wao si lolote si chochote!

Somo: usiwe mwepesi kushabikia mambo usiyoyajua kwa undani kwa kuwa tu yanafanywa na wazungu

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %