
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo amefanya mahojiano na WABONGO UGHAIBUNI MEDIA katika kipindi maalumu Cha Diplomasia ya Uchumi “ECONOMIC DIPLOMACY”.
Mahojiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania Rome.
Katika mahojiano haya Mh Balozi amezungumza mengi kuhusu utekelezaji wake wa sera ya Diplomasia ya Uchumi, mikakati yake ya kufungua fursa za uwekezaji Pamoja na kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nchini Italy. Mh Balozi ametoa mwanga kwa Watanzania jinsi gani wanaweza kufaidika kibiashara Kupitia Balozi zetu.
Wabongo ughaibuni Media WU®, wanakuja na kipindi hiki maalumu kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha ni jinsi gani Kupitia Balozi zetu Nchi inaweza kufaidika kiuchumi na kufungua fursa mbalimbali za kibiashara na hasa kuonyesha Kazi za Mh Rais kimataifa Kupitia wawakilishi wake nje ya nchi.
Wabongo ughaibuni Media, wanategemea kuendelea na kipindi hiki Cha “ECONOMIC DIPLOMACY” katika nchi za Ufaransa, Belgium, Germany, UK, Austria, Turkey, Russia na China.
“Ili kuwa wa kwanza kupata notification kila mara kufuatilia mfululizo wa vipindi hivi subscribe na bonyeza kengele.”
WABONGO UGHAIBUNI MEDIA PRODUCTION LIMITED WU®








