WU® MediaPRODUCTION LIMITED
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewataka wakuu wa mikoa kote nchini kuacha urasimu na kuharakisha ugawaji wa pembejeo kwa wakulima.
Komredi Shaka ametoa maagizo hayo baada ya kusikia malalamiko ya wananchi katika kijiji cha Lukuledi mwanzoni kwa ziara yake ya siku nne mkoani Mtwara.
Wananchi hao walilalamika walilalamikia kuchelewa kupewa pembejio za zao la Korosho.
“Hili nalisema kwa wakuu wote wa mikoa waondoe urasimu na wagawe haraka pembejei hizi… mh mkuu wa mkoa naomba uunde kamati haraka kugawa pembejio hizi” alisema Shaka
Amesema serikali ya ccm inayongozwa na Rais Samia imeamua kugawa bure pembejeo hizo kwa wakulima hivyo kuzichelewesha ni kufifiisha nia nzuri ya serikali.
“Asubuhi Mkuu wa Mkoa alinipa taarifa kwamba pembejeo zimeshafika,kwa hivyo niwatake Serikali ya Mkoa wa Mtwara waache urasimu, ndani ya wiki moja pembejeo ziwe zimetoka, tunataka wananchi wanufaike na hatua ya Rais Samia ambaye ameamua kutoa bure pembejeo za kilimo, lengo kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao,” alisema Shaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Meja Jenerali Marko Gaguti, amesema amepokea maelekezo hayo na atakwenda kuyafanyia kazi.