0 0
Read Time:5 Minute, 57 Second

WUยฎ MediaPRODUCTION LIMITED

SHIVJI ON THE LOLIONDO/NGORONGORO LAND OWNERSHIP CRISIS

Kwa heshima na taadhima pokea barua yangu nikikutumia kwa nia njema na katika kutekeleza wajibu wangu kama mwananchi na mwanazuoni kwa mujibu wa ibara 26 ya Katiba.

Issa Gulamhussein Shivjiย (born 1946) is aย Tanzanianย author and academic, and one of Africa’s leading experts on law and development issues. He has taught and worked in universities all over the world. He is a prolific writer and researcher, producing books, monographs and articles, as well as a weekly column printed in national newspapers.”


Awali ya yote nakutakia maisha marefu yenye afya njema na furaha tele ili uendelea kutuongoza, kwa busara na hekima na kwa kulinda Katiba yetu bila hofu au upendeleo.

Katika sakata la Loliondo na Ngorongoro nimesikia mara kwa mara mawaziri husika wakitamka bungeni kwamba ardhi yote nchini ni mali ya umma na hakuna mwe-
nye ardhi. Kwa heshima, kwa mao- ni yangu, tafsiri hiyo ya sheria sio sahihi.

Ni kweli kwamba Sheria ya Ardhi inasema ardhi yote nchini ni ‘public lands’ yaani ardhi ya kiumma na imewekwa mkononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi. Kifungu 4, kifungu kidogo 1, cha Sheria ya Ardhi 1999 (sura 113) kinatamka kwamba ardhi yote nchini Tanzania itaendelea kuwa ardhi ya kiumma na itaendelea kuwa mkononi mwa Rais kama mdhamini
kwa niaba ya wananchi wa Tanzania. Kifungu hiki kinahitaji ufafanuzi. Kwa nini sheria inatumia neno
‘itaendelea”? Kwa sababu tangu mwaka 1923, sheria ya ardhi ya kikoloni ili tamka kwamba ardhi yote nchini ni ardhi ya kiumma na ikawekwa mkononi mwa Gavana.
Mfumo huo haukubadilika baada ya Uhuru isipokuwa tu badala ya neno ‘Gavana’ ikawekwa neno ‘Rais’. Mfumo huu umeendelezwa na Sheria ya Ardhi ya 1999 ambayo
ni sheria mama kuhusu mfumo wa umilikaji ardhi Tanzania.

Nisisitize jambo moja. Kifungu hiki hakisemi wala hakimaanishi, kwamba ardhi ni mali ya umma. Kinaainisha tu ardhi kama ardhi ya kiumma na sio tamko la umilikaji
ardhi. Kuna tofauti ya msingi kati ya kuainisha ardhi na kumilikisha ardhi. Neno ‘mali’ halipo kabisa katika kifungu hiki. Kwa hivyo, ardhi sio mali umma wala ya Rais wala ya Serikali. Kama hivyo ilivyo, basi ardhi
ni mali ya nani?

Kifungu cha 4, kifungu kidogo cha 3, kinasema kwamba wote waliokuwa wanakalia ardhi kabla ya Sheria ya 1999 kwa hati rasmi au kwa mujibu wa mila na desturi,
wataendelea kukalia ardhi hiyo. Kifungu kidogo hiki kinaendelea kusisitiza kwamba ukaaji wa ardhi chini ya hati rasmi au kwa mujibu wa mila na desturi itahesabiwa
kama mali (‘property’). Katika kifungu hiki mara ya kwanza sheria inatumia neno mali, kwa Kiingereza, property. Kifungu hiki kinaendelea kusisitiza kwamba pamoja na ukaaji kuwa mali, pia matumizi ya ardhi kama malisho ya mifugo kwa mujibu wa sheria za mila na
desturi inahesabiwa kuwa mali.

Moja kwa moja, sheria imeweka wazi kabisa kwamba matumizi ya ardhi na wafugaji kwa malisho ya mifugo yao inahesibiwa kama mali, yaani property. Sasa ardhi ni mali ya nani? Ardhi ni mali ya wenye hati rasmi au jamii au kaya au watu binafsi wanaokaalia ardhi kwa mujibu wa mila na desturi, pamoja na wafugaji ambao hutumia ardhi
yao kama malisho.

Reports) [1995] T.L.R. 80).
Ninanukuu kipengele muhimu cha uamuzi huo:
“Haki za ardhi chini ya mila na desturi, ingawa kwa uhalisia wake ni haki ya kukaa na kutumia
ardhi, bado ni mali [property] ambayo inalindwa na ibara 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utwaaji wa haki za mila bila fidia ya haki inazuiliwa na Katiba.” (uk. 81) Kama kweli hii ndio sheria ya nchi kwa nini upotoshaji wa “Haki za ardhi chini ya mila na desturi,
ingawa kwa uhallsla wake ni hakl ya kukaa na kutumia
ardhi, bado ni mali [property] ambayo inalindwa na Ibara 24ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utwaaji wa haki za mila bila fidia ya haki inazuiliwa na Katiba.” (uk.HABARI 9

Hao ndio wenye ardhi, sio umma wala Rais wala Serikali.
Kwa hivyo, sio sahihi kabisa kusema kwamba ardhi ya Tanzania haina wenyewe. Tafsiri ya sheria niliyotoa hapo
juu iliwekwa wazi na mahakama ya juu kabisa nchini, Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya Lohay Akonaay na Joseph Lohay iliyoamuliwa mnamo mwaka wa 1994 na kuchapishwa rasmi katika Ripoti za Kesi, Tanzania (Tanzania Law 81)mawaziri umeendelea bila kupingwa au kusahihishwa? Kwa nini
wanapotamka kwamba ardhi ya Tanzania ni mali ya umma hawabanwi, (kama wanavyobanwa waheshimiwa wabunge wengine), kunukuu kifungu cha she-
ria kinachosema ardhi ni mali ya
umma?

Kwa kadri ya uelewa wangu, mwenye dhamana na wajibu wakutoa tafsiri ya sheria bungeni na kushauri wabunge (bila kujalivyama vyao) na Bunge juu ya sherรญa ni Mwanasheria Mkuu. Kama tunajua, hatimaye kauli
ya mwisho juu ya tafsiri ya sheria ni Mahakama lakini anyetakiwa kutoa tafsiri ya sheria bungeni pale ambapo kuna ubishi ni Mwanasheria Mkuu, sio Spika wala mbunge mwingine yeyote hatakama yeye ni mwanasheria.

Kwa kuwa tafsiri ya sheria iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Akonaay imewekawazi kwamba haki ya kumilikiardhi chini ya mila na desturi ni mali inayolindwa na ibara ya 24 ya Katiba na kwa kuwa kauli
ya Mahakama ya Rufaa ni kauli ya mwisho, basi ardhi ya jamii ya wafugaji wanaoishi na kutumia ardhi yao katika maeneo ya Loliondo na Ngorongoro kwa malisho, haiwezi kutwaliwa na Serikali bila kufuata taratibu za sheria zilizowekwa katika Sheria ya Utwaaji wa Ardhi, sura 118
(Land Acquisition Act).

Mwenye mamlaka kutwaa ardhi ni Rais na hana budi afuatehatua zote za kutwaa ardhi zilizotajwa katika Sheria, sura 118. Kinyume na hii, uhamishaji wa wenyeji kutoka maeneo haya, kwa kulazimishwa au kwa
hiari, ni batili na moja kwa mojaunavunja sheria za nchi na haki za msingi za binadamu kama zilivyoorodheshwa katika Katiba.

Kwa kuhitimisha barua yangu, Mheshimiwa, naomba niju-
muishe hoja zangu kama ifuatavyo:
Mosi, ardhi yote ya Tanzaniani ardhi ya kiumma. Tamko hilila sheria ni tamko la kuainisha ardhi sio tamko la kumilikisha ardhi kwa Serikali.

Pili, ardhi imewekwa mkononi mwa Rais kama dhamana. Kazi yake kama mdhamini ni kuhakikisha kwamba ardhi inawanufaisha wananchi na sio vinginevyo.
Kisheria na kwa mujibu wamila za kisheria tunazozifuata,
mdhamini (trustee) ana wadhifawa kipekee na ni nzito.
Uhusiano kati ya mdhamini na mnufaishwa ni uhusiano mahsusi ambao sheria na mila inaangalia
kwa jicho la kipekee.

Tatu, umiliki ardhi wa mojakwa moja unabaki kwa wenye
hati rasmi na watu au kaya au jamii kwa mujibu wa mila na desturi.

Nne, umilikaji wa ardhi kupitia mila na desturi ni mali (property) na unalindwa na Katiba.

Tano, ardhi ya mila haiwezi kutwaliwa na Rais bila kufuata
hatua zote zilizoainishwa katika Sheria ya Utwaaji wa Ardhi (LandAcquisition Act).

Mwisho, kutokana na mambo ya msingi niliyotaja hapo
juu, wakazi wa Ngorongoro na Loliondo, hususan jamii za wafugaji, hawawezi kuondolewa kutoka ardhi yao bila kufuata taratibu za kisheria na kwa sababu mahsusi ambayo lazima ijulikane na kujadiliwa hadharani.

Mheshemiwa Rais, sisi sote, wananchi pamoja na Serikali tujiulize: Je, uondoshwaji wa wananchi katika ardhi yao, ambayo ni uhai na urithi wao, kwa minajili ya kupisha wanyama pori ili kampuni za uwindaji, kwa mfano,
zifanye shughuli zao bila kubughudiwa na wananchi, ni kwa manufaa mapana ya umma wa Tanzania? Nakiri sina jibu isipokuwa swali hili linanikosesha usingizi.

Nakutakia kila la kheri Mheshimiwa Rais
Issa Shivji ni Profesa Stahiki
(Professor Emeritus). Shule
Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %