WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amezungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohra (Dawoodi Bohras) duniani, Syedna Muffaddil Saifuddin na kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa dhehebu hilo kuja kuwekeza Zanzibar.
Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Zanzibar ambapo kiongozi huyo wa Madhehebu ya Bohra akiwa na ujumbe wake walionyesha azma ya kuendedelea kumuunga mkono Rais Dk. Mwinyi katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Dk. Mwinyi alimweleza kiongozi huyo fursa mbalimbali zilizopo Zanzibar pamoja na mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya Biashara na Uwekezaji.
02 Julai, 2022
Ikulu, Zanzibar