
KWA LUGHA RAHISI NCHI YA SRI LANKA IMESHAJIPIGA MNADA YENYEWE!
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 18,2022.
Kwa lugha rahisi kabisa,mpaka dakika hii,unaweza kuitimisha kuwa, Nchi ya Sri Lanka masikini imeshajipiga mnada yenyewe kwa mashirika ya fedha ya kimataifa yaani WB,IMF na Beberu mpya duniani Uchina!
Baada ya wakopeshaji wa nje “foreign lenders” kuikopesha Sri Lanka zaidi ya USD 51Bilion na kwa mara ya kwanza Sri Lanka kushindwa kufanya marejesho mwaka Jana, June 2021, baada ya Hazina yake kuu kuwa kavu baada ya kushindwa kulipa USD 7 Bilioni kwa mwaka 2021 bado mabeberu wanataka “kuibaka” tena Sri Lanka!

Mpaka mwaka jana,Banki ya Dunia ilikuwa ikiidai Sri lanka asilimia 20 ya deni lote la Sri lanka wakati Japan na China pia zilikuwa zinaidai Sri lanka karibia asilimia 20 la deni lote la Sri Lanka!Kwa kifupi, tumesema mpaka dakika hii, Sri Lanka haiwezi kulipa chochote na mabeberu wanajua fika, lakini bado wanataka “kuipiga”mnada Nchi hiyo masikini!
NINI KINAENDELEA KWA SASA DUNIANI KUHUSU SRI LANKA?
Banki ya Dunia,IMF,China na India zinataka kuipiga mnada Sri Lanka baada ya kutangaza mkopo mwingine kwa Sri Lanka hivi karibuni!Banki ya Dunia pekee inataka kuikopesha tena Sri Lanka kiasi cha USD 600 Milioni,China inataka kuikopesha tena Sri Lanka kiasi cha USD 1.6 USD Bilioni,hivyo hivyo IMF USD mkopo wa USD 3 Bilioni na hivyo hivyo kwa India, USD 1.9 Bilioni!
Na hapa ndio unaweza kutafsiri ile Theory ya Professor Nurke ya “VICIOUS CYCLE OF POVERTY” kwamba Nchi za ulimwengu wa tatu zimekuwa zikishindwa kutoka katika umasikini kutokana na kufungwa kimkakati kwenye mnyororo wa umasikini na Nchi za mabeberu na mashirika yao ya fedha!
Usingeweza kutegemea kuwa baada ya mashirika haya kushindwa kulipwa na Nchi ya Sri Lanka lakini bado tena yanataka kuibaka tena Nchi ya Sri Lanka,Shame!
Hii ina maana gani?Nchi ya Sri Lanka, angalau itatumia miaka angalau 100 mpaka kuweza kulipa madeni haya yenye riba kubwa hivyo kudumaza kabisa maendeleo yao kwa miaka 100 mbele!
NINI CHA KUJIFUNZA HAPA SISI KAMA TANZANIA?
I.Lazima tukae chini kwa pamoja tuwekane sawa kuhusu deni/madeni yetu dhidi ya IMF,WB na taasisi zingine!Sri Lanka imejikuta imefikia hapo kutokana na maamuzi wanasiasa tu na kuifanya Nchi sasa kupigwa mnada!
Ni wazi kuwa mikopo ya IMF & WB haina nia njema kwa Nchi zetu sababu katika hali ya kawaida kamwe usingetegemea taasisi hizi “zicommit” kiasi kikubwa tena cha fedha kwa defaulter Sri Lanka!
II.Moja ya sababu ya Sri Lanka kukumbwa na balaa la madeni ni kutumia fedha za mikopo hiyo katika kuwekeza katika kitu kinaitwa Social Safety Net kwa huku kwetu Tanzania unaweza ukaita TASAF!Je,kuna haja na sisi tufikirie kuikagua TASAF na kuona kama malengo yake yanatimia?
Mikopo tunayochukua WB yaani World Bank kwa ajili ya kuwezesha kaya za kitanzania masikini je, imetusaidia?Nchini Sri Lanka imewahi kutekeleza miradi kama hii kupitia mikopo kutoka IMF!
III.Kama Nchi ya Sri Lanka yenye GDP ya 80.71 USD Bilioni na Population ya 21.92 Milioni inakwama kulipa mkopo kwa kifirisika huku sisi Tanzania tukiwa na GDP ya karibia 60 USD Bilion tu na Population ya karibia 60 million zaidi ya Nchi ya Sri Lanka!Je,tuna kitu cha kujifunza hapo?
Deni la nje la Tanzania ni karibia 26 USD Bilioni kwa mujibu wa takwimu za mwaka August 2021 huku deni la nje la Sri Lanka ni 35 USD Bilioni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 tofauti ya USD Bilioni 9 tu!
Nadhani hapa pana kitu cha kujifunza kwa haraka haraka na kama tutakaa kimya na kuendelea “ku top-up” na sisi tunaweza kuingia katika kitu kinaitwa “Debt Trap” kama ambavyo Sri Lanka wamejikuta wamo!
Hata tusije tukajidanganya kuwa mkopo wa IMF & WB Banki unaweza ukawa na unafuu kwetu!IMF & WB sio Baba zetu wala wajomba zetu hivyo tunahitaji umakini mkubwa katika kudeal na mikopo yao kuanzia sasa!
Sijasema Mama ASIKOPE,HAPANA lakini nasema, lazima tukae chini sasa tuambiane na kuelimishana kama kweli Tanzania tupo salama kwa kiwango hicho tunachoambiwa na kaka yangu Mwigulu Nchemba,Waziri wangu wa fedha!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Munduli Arusha, Mhadhiri Msaidizi Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255746726484.








