WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Na Mwandishi wetu
Taarifa zilizo tufikia muda huu usiku, Mtanzania pichani aliyetambulika kwa Majina MUSTAFA MUNAWAR KARIM amekutwa amefariki nyumbani kwake katika kitongoji Cha Pinetamare CastelVolturno wilaya ya Caserta nchini Italy.
Marehemu alikuwa hajaonekana kutoka nyumbani kwake kwa takriban siku tatu, ndipo majirani walipoamua kuita police ili kujiridhisha usalama wake. Mpaka muda huu Bado taratibu za vyombo vya usalama zinaendelea na mwili Bado haujachukuliwa. Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania nao wamefika katika tukio wakiongozwa na Katibu Dada Cecilia Lemmah.
“Innalillah wainna illah raj uun”