0 0
Read Time:7 Minute, 22 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

BENITO MUSSOLINI WA ITALIA NA UJANJA UJANJA WAKE HADI KUINGIA MADARAKANI NA KUGEUKA FASHISTI

Maovu na Ubaya wa utawala wa Stalin wa Urusi kipindi hicho ulikuwa haufahamiki kote kote nje na ndani ya Umoja wa Kisovieti ,na wageni wengi walibakia kuwa mashabiki wa ukomunisti. Kuna siku moja mtalii mmoja wa Italia alirudi kutoka Urusi akaeleza habari za Urusi na kwamba ameona jinsi Urusi ya Stalin, inavyofanya maovu na utawala wake.

Hilo liliwapa hofu watu wengi, wakajawa na hofu na hayo mambo mapya ya ukatili yanayoendelea huko Urusi chini ya Joseph Stalin, ufashisti ukaendelea kukua ,ufashisti ulionekana kama mbadala wa ukomunisti na ni mawazo tofauti na harakati za kisiasa ambazo ni mpya.

Benito Mussolini alizaliwa huko Dovia mwaka 1883 ,Mussolini alikuwa katili na kijana shupavu, alihitimu chuoni kama mwalimu lakini baadae akabadili fani na kuwa Mwandishi wa habari ,mwanzo alikuwa akifuata Sera za Ukomunisti ,na mara kwa mara aliongoza migomo iliyomfanya aishie jela, kiujumla alipendelea jeshi liwe linatatua matatizo ya Serikali.

Mara anapoongoza maandamano mijini alikuwa akitishia kuuangusha utawala wa Meya, alikuwa akimtimsha kwamba atamrusha nje ya dirisha kama bei ya maziwa isingepunguzwa.
Mwaka 1914 aliwahi kuongelea habari za kuung’oa utawala wa Serikali ya Italia kwa kutumia jeshi, Benito alikuwa ameweka mikakati yake kichwani kwake kwamba ili kuung’oa utawala yapo mambo ya aina mbili ya kuyafuata la kwanza ni ; kutumia kundi la watu maarufu na pili ni kwa kutumia vurugu.

Vita Kuu ya kwanza ya dunia ilimfanya Mussolini akate tamaa juu ya itikadi ya Ukomunisti , kwasababu Wajamaa wengi wa nchini Italia walikuwa wapo kinyume na vita hiyo kwasababu waliamini ilipiganwa ili kuwapa utajiri zaidi Mabepari. Mussolini kwa upande mwingine alijithibitishia kuwa vita dhidi ya Australia- Hungary ingeipa Italia maeneo ya Trentino na Trietse ,Tamaa hii ya kulipanua jimbo la Italia ilimfanya kuhalalisha vita na pia kutukuza mapigano.
Kwenye hotuba zake na maandishi aliyoandika aliyapigia kelele mambo hayo kwa vitendo , Waitalia wengi hawakupenda mambo ya vita na ugomvi lakini Mfalme pia alijazwa na ndoto za utukufu.

Mwisho wa siku Serikali ikakubali matokeo na kutangaza kupigana vita upande wa Muungano. Mussolini akaharakisha kujiunga vitani na kuona ni jinsi gani ilivyo rahisi kwa sauti za raia maskini kupata nguvu ya kukubalika kwa mambo yao. Mussolini alikuwa askari jasiri akapigana vita mstari wa mbele mpaka akajeruhiwa kwa ajali ya mlipuko wa bomu ,akarudi nyumbani kujiuguza na akapumzika kama askari shujaa aliyejeruhiwa.

Kwa muda mrefu baada ya kujifikiria na kuona kuwa yeye ni mtu wa muhimu alianza kutembea kwa mikongojo kwa tabu ili apone haraka, katika hotuba zake alipendelea kujiita ” majeruhi”. Wakati huohuo aliendelea kusisitiza kwamba nchi ya Italia inachohitaji ni Kiongozi Dikteta”zinahitajika Juhudi za kutosha kusafisha uchafu nchini humo”

Mbinu na matendo yote ya kifashisti, vurugu ,udikteta , utukufu wa vita, vyote hivi vilikuwa ndani ya akili ya Mussolini ,kilichokuwa kimebakia kilikuwa ni kubuni jina na kupanga Chama chake ,Machi 23, mwaka 1919 ,Mussolini akaunda chama cha ” Fascio di Combattimento” (yaani kundi la mapigano) huko Milan.
Hapa lilianzishwa kundi la watu ambao ni mafashisti tu, watu muhimu tu waliotamba kwa kusema kwamba wameungana pamoja kama shoka na gogo la ufashisti, kundi ambalo lilimaanisha nguvu ya Roma ya Kale.

Kama ilivyo kwa nchi nyingi za Ulaya baada ya Vita kuu ya dunia ,Italia Kwa muda mfupi ilisumbuliwa na vita, ikawa na madeni mengi ,palikuwa na mamilioni ya watu wasiokuwa na ajira ,zaidi ya watu 150,000 walizurura na kuleta tabu mitaani ,kwa hali hiyo wazo la Ukomunisti lilisambaa haraka.

Bendera nyekundu za kikomunisti zilizagaa kwenye kambi za mijini na kwa wasovieti wa ndani ya nchi ,sasa mambo yakawa ni moto ,baada ya kundi maarufu lililoitwa “mashati meusi” kuibuka, mpambano ulikuwa wa makundi kati ya wakomunisti na mafashisti, likawa jambo la kawaida kwa kuonekana kila kona kuna mapigano,watu waliuawa na kupigwa vibaya sana ,wengine wakajijaza mafuta au kula vyura walio hai.

Maisha ya kawaida yaliharibiwa, migomo na maandamano na uvamizi wa kambi za jeshi ,stesheni za Reli ,na mabenki vilijaza vichwa vya habari kwenye magazeti. Pamoja na yote hayo karibu watu 3,000 waliuawa katika mapigano hayo ya mitaani kwa miaka miwili . Ni viongozi wa kikomunisti tu walioshutumu vurugu hizo za kifashisti ,wengine waligundua mengi wakakiunga mkono Chama cha Mussolini ,kwa mfano; wamiliki viwanda , na wamiliki ardhi waliotaka kuwekeza viwanda na ardhi zao. Kwa upande wa wakatoliki wao waliogopa dini yao inawezakuharibiwa na Ukomunisti usioamini uwepo wa Mungu .

Watu waliokuwa tabaka la kati waliopenda Sheria na amani waliwasaidia wananchi wa Italia,vurugu na ukatili uliofanywa na kikundi cha kifashisti ulipuuzwa na Mfalme, Jeshi pamoja na Polisi ,bali vurugu za wafuasi wa Ukomunisti waliadhibiwa vikali.

Tarehe 28, Oktoba mwaka 1922 msururu wa maandamano wa kikundi cha “Mashati Meusi “ulianza mwezi Machi huko Roma, hawakuwa wakitaka vita kama ilivyoonekana hapo mwanzo. jeshi likawatawanyisha, lakini Mfalme alionekana akipendelea ufashisti zaidi, kama njia ya kuukataa ukomunisti, akamwalika Mussolini Ikulu na kumteua kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya vyama vyote ,akawa anaishi mbali huko Milan. Kiongozi wa chama cha kifashisti, Mussolini, hakuamini macho yake kwa uteuzi huo, alijiona ana bahati kubwa.

Alipoingia madarakani Mussolini alianza kujenga mawazo yake binafsi kama ni “Mtu pekee”, Waitalia walikaribishwa kuungana nae ili kuongeza juhudi za kuifanya Italia kuwa kubwa kama ilivyokuwa kipindi cha Roma ya Kale.

Picha na Filamu mara nyingi zilimuonyesha kiongozi huyo (Duce II yaani, Kiongozi wa Chama cha kifashisti II) kama alivyojiita mwenyewe ,akifanya kazi kwa bidii katika kiti chake au yupo bize nje akikata miti au anachimba mifereji, wakati mwingine anaonekana yupo tumbo wazi na kifua chake kipana kinatoka jasho sababu ya kazi ngumu .

Kwenye matukio mengine anaonekana kavaa sare nadhifu na nzuri huku akiangalia gwaride la kijeshi huku akiwa na sura yenye umakini sana, kila Usiku taa yake ya ofisini iliachwa ikiwaka kutoa ishara kwamba alikuwa bado yupo bize akifanya kazi. Alijitangaza kuwa yeye ni “Kijana wa watu” sababu Baba yake alikuwa mfua chuma ,kipindi hicho busara na ujanja wake vilisisitizwa, wakati mwingine alipigwa picha akishinda mchezo wa drafti ,mchezo ambao alikuwa hajui hata kuucheza.

Yote hayo yalikuwa ni usanii tu, Serikali ya Mussolini iliweza kujenga madaraja, Reli, mifereji, Hospitali ,na shule. Barabara mpya zilijengwa kati ya miji mikubwa, mabwawa yalikaushwa na misitu ilipandwa, wageni wengi wakaanza kumkubali Mussolini ,wakatoliki wakafurahishwa mara aliposaini mkataba wa Lateran na Concordat na Papa mwaka 1929.

Tangu mwaka 1870 mapapa Wengi waliopita walikataa kutambua ufalme wa Italia sababu Mfalme alichukua jimbo lililokuwa likimilikiwa na wao. Sasa Papa alitambuliwa kama Kiongozi wa jiji la Vatican .Roma ( eneo la takribani hekta 40) na Roma ya kikatoliki ilitangazwa kuwa nchi ya kidini.

Ukweli uliweza kubadilisha mawazo ya watu wengi, mwanzo Mussolini alikuwa maarufu sana, mahitaji yake na amri za mara kwa mara ,nidhamu ,kujitoa kafara, na kazi ngumu vilivyowafurahisha watu hapo mwanzo viliwavunja moyo Kwa vita alivyovipigania.

Lakini baada ya mauaji ya kikatili ya mafashisti wa ujamaa ,Giacomo Matteotti mwaka ( 1924) baada ya kuanza kuua Mussolini akaja kupoteza umaarufu wake, bila vurugu na ujanjaujanja Mussolini asingeshinda uchaguzi wa mwaka 1924. Ilipangwa kwamba Chama ambacho kitaongoza kwa kura kitakuwa moja kwa moja kimepata mbili ya tatu ya viti bungeni.

Ili kupata viti hivyo watu wa Mussolini waliwapiga wanasiasa wapinzani ,baada ya ushindi huo Mussolini aliachana na masuala ya Demokrasia ,Mfalme alibakia ndiye kama mkuu wa nchi lakini asiye na nguvu Lakini bunge pia likapoteza nguvu za kutunga sheria, vyombo vya habari vilikandamizwa na kukaguliwa habari zote kabla ya kuchapishwa ,bali vilichapisha nini alichotaka fashisti tu, Jeshi la zamani la Squadristi likageuzwa kuwa la mgambo wa fashisti likafanya kazi kama jeshi la Polisi saidizi.

Wafanyakazi walifanya kazi kwa masaa mengi na kunyimwa haki ya kugoma, watoto walitakiwa kujiunga kwenye ” Fascist Youth” maarufu kama Ballila. Wapinzani wa utawala walitupwa kwenye jela maarufu kama (Concentration Camp) Mussolini aliamini Neno “Ukombozi” ni zaidi ya kama Mungu aliyeoza.

Siku baada ya siku waitalia walihimizwa kuwa watu wa vita ,hata Jeshi la watoto ( Ballila) lilibeba bunduki za midoli, Walifundishwa kupuuza majadiliano huru na Uhuru wa kuchagua. Walikumbushwa juu ya ukubwa wa Roma ya Kale na kutakiwa kuhitaji himaya mpya ya waitalia. Watoto wa shule walifundishwa kuimba ” Mussolini siku zote yupo sahihi”. Hivyo sio moja kwa moja kwamba Ukomunisti ulisaidia kuundwa kwa mfumo wa kidikteta bali ulisaidiwa na Mabepari na tabaka la kati ambalo Marx alililaani.

Hadi mwaka 1930 makundi ya kisiasa ya kigeni hasa hasa Nazi chini ya Hitler wa Ujerumani ,walikuwa wakiiga mbinu za Fashisti Mussolini, maonyesho yake ya magwaride uwanjani, beji wanazovaa ,maringo ya Fashisti Mussolini na ubabe wake, palikuwa na tofauti kati ya Hitler na Chama chake cha NAZI kwasababu Hitler aliutukuza sana ” Ubaguzi wa rangi “.

Ujerumani na wanachama mafashisti wa Hispania waliipenda dini ya Kikatoliki ya Roma badala ya kuiabudu Roma ya kale, vinginevyo wote walikuwa wasiovumilia vurugu , na wote walichukia vyote viwili Demokrasia na Ukomunisti ,wote waliabudu Kiongozi maalum , Ukomunisti kivitendo ilikuwa ni sera ya vurugu inayoogopesha na ya kidikteta, Ufashisti wenyewe uliamini usawa ni kitu kibaya…

Imesambazwa na Mpoki Buyah Kaminah Mwandagasya mpoki.buyah@gmail.com Ukuu WA MWAAFRIKA NA WABABE WA KIVITA NA HISTORIA YA DUNIA..

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %