0 0
Read Time:1 Minute, 53 Second

AMPONGEZA WAZIRI MCHENGERWA NA ZAIDI KWA UPEKEE AMPONGEZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH SAMIA SULUHU HASSAN.

MHE. ANTHONY JOHN MTAKA 

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Simbu ameshinda medali ya Fedha kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayofanyika nchini Uingereza.

Mambo Makuu na ya Muhimu katika ushindi huu,Moja nazipongeza juhudi binafsi za mchezaji na walimu wake waliomwezesha kufanya vizuri,Mbili ni somo la umuhimu wa kuwekeza kwa mda mrefu katika kulea na kujenga vipaji,naweza sema imemchukua Simbu miaka 10 katika kufanya mazoezi,mbio za majaribio nk mpaka kuweza kushinda medali na kukata kiu ya watanzania ambao kwa miaka Mingi medali katika riadha ilikuwa historia.

Tatu na kubwa katika Yote ni Namna ambavyo serikali kupitia utashi na utayari wa Waziri anayehusika na Michezo kaka yangu Mchengerwa na Katibu Mkuu Dr.Abbasi walivyoweza kutafsiri maandalizi ya timu za Taifa kwa vitendo,naweza sema kwa miaka 50 toka tupate uhuru huenda Mh.Mchengelwa akawa ndiye waziri Bora wa Michezo ambaye ameongea kwa vitendo vinavyotekelezeka kuhusu nini maana ya timu ya Taifa,nini maana ya kujiandaa na nini cha kufanya ili wachezaji wafanye vizuri,ameondoka kwenye ubora wa hotuba na kugawa Bendera kwa timu(Maana zamani wachezaji wanajiandaa kwa nguvu zao halafu mwisho wa siku wanakabidhiwa Bendera na hotuba motomoto za kwenda kuwa Wazalendo)

Mh.Waziri Mchengerwa na timu yake ya wizara,BMT na kurugenzi ya Michezo,wamekuwa sehemu ya kambi,Maandalizi na hata ahadi ya nini watatoa kwa wachezaji watakao fanya vizuri,Nakupongeza sana kaka yangu,umeitendea haki michezo,umeitendea haki Riadha,na kwa Mwendo huu Kenya na Ethiopia tunaweza kuwashinda Olympic Ijayo na Mashindano mengine yajao ya kimataifa ,katika riadha na michezo Mingine.

Above All nampongeza kwa Dhati Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyothamini vipaji ,utayari wake umeongeza morali kubwa kwa timu zote za Taifa,nampongeza Balozi Dr.Migiro ambaye wakati wote amekuwa sehemu ya Riadha,leo ni mara ya pili anashiriki hamasa ya Simbu akiwa Uingereza.

Ushindi wa Simbu ni heshima kwa nchi yetu,heshima kwa wanamichezo na ni heshima kwa JWTZ ambao ni waajiri wake.Hongera sana sana sana.Mungu akusimamie,na Kwa Heshima ya Ushindi wake nikiwa sehemu ya walezi wake Ntampa zawadi ya Kiwanja Ndani ya Jiji la Dodoma kuenzi Medali hii ya Jumuiya za Madola.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %