0 0
Read Time:42 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

BAADA ya ngojangoja ya muda mrefu, hatimaye bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo ametajwa kurejea ulingoni kuzichapa na Liam Smith Septemba 3, mwaka huu.

Mwakinyo atapigana na Smith ambaye ni raia wa England kwenye pambano hilo linalotajwa kuwa la ubingwa wa dunia wa uzito wa super welter likiwa na raundi 12 jijini Liverpool, England.

Smith ni bondia namba moja Uingereza akishika nafasi ya sita duniani kwenye uzito huo huku akiwa na nyota tano, atapambana na Mwakinyo anayeshika nafasi ya 37 kwa sasa baada ya kuporomoka hivi karibuni na kuwa na nyota tatu na nusu.

Mwakinyo ambaye ameshuka ubora wa viwango kutokana na kutopanda ulingoni kwa muda mrefu, endapo atashinda pambano hilo ataandika historia mpya zaidi ya ile ya mwaka 2018 alipomchapa bondia namba nane wa dunia, Sam Eggington na kupanda hadi ya nafasi ya 14 ya uzani huo duniani.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %