WU® MediaPRODUCTION LIMITED
“Huu ni ujumbe uliondikwa na Admin wa group la hadhi Maalumu kwa Wana group”
Kwa kifupi tu dhumuni la group hili ni kwa wale waumini wa HADHI MAALUMU tu, wale wenye mrengo wa nje ya HM mnaruhusiwa kusoma ili mjue umuhimu wa HM.
Kwa kuwa mmeshindwa kuheshimu maamuzi ya serikali kutoa HM na mnabakia kung’ang’ania DC na Mahakama, basi hapa sio sehemu yenu ya kuchat bali mtabakia kusoma tu.
Wanagroup wa HM wataendelea kuchat na kukumbushana na kuelimishana huku wakiendelea kuvuta subira ya kusubiri jambo lao muhimu katika maisha yao na familia zao.
Hii itasaidia kuepusha kujaziano wino wa DC ambayo tunajua wazi sio kipaumbele cha sasa kwa serikali.
Draft ya Hadhi Maalum bado ni Document yenye Mapendekezo ambayo yanafanyiwa kazi na Serikali. Ikifika mwisho, then itatangazwa na kuwa Public. Ila kwa kuwa wanadiaspora walishatoa maoni yao kwahiyo HM inakwenda kujibu most of your long time needs. No one will ever want again DC after SS is fully granted.
Mapendekezo yalishatolewa na wanadiaspora wote duniani waliotekeleza zoezi hilo
Na kupitia maoni na mapendekezo hayo ya Diaspora na wadau wengine, Hadhi Maalum ikaanza kuandaliwa. Imetokana na maoni ya Diaspora.
Kimsingi Hadhi Maalum ni jambo la heri litakalowanufaisha Diaspora wote wenye asili ya Tanzania. Na mchakato wake una baraka zote za Serikali na Viongozi wake. Na hauna changamoto kwa sababu unalenga kuwakumbatia Diaspora wote wenye asili ya Tanzania.
Ndugu zangu Wanadiaspora.
“Baniani Mbaya Kiatu chake Dawa”. Maana yake ni nini? Kuna baadhi ya michango yetu inaashiria kama baadhi yetu hatuna kabisa imani kuwa ni kweli Serikali ita grant Hadhi Maalum. Baadhi yetu, tunafikia hata kutaka kudhihaki kwamba ni kitu hakina uhalisia. Lakini, naomba tukumbuke yafuatayo:
- Serikali yenyewe, tena kwa utashi na mapenzi yake makubwa kwetu Diaspora ndio iliamua kututangazia kwamba imesikia maombi yetu na itatuletea Hadhi Maalum ili kurahisisha masuala yetu mbalimbali. Hatukuilazimisha wala hatukuomba.
- Hadhi Maalum sio dhana ngeni Duniani. Nchi kadhaa duniani kama Ethiopia, India na nyinginezo, ambazo hazijakubali DC, zimeanzisha utaratibu kama huo. Nasi Serikali yetu iliona ni vema kutuandalia kitu kama hicho;
- Lakini tukumbuke kuwa masuala mengi ambayo tuliyaomba Serikali iya grant kupitia HM, yanazo Sheria za zinazoyakataza. Mathalani ombi la haki ya kuingia nyumbani bila ya Visa na kukaa bila kikomo; Haki ya kurithi, kurithisha Mali na kumiliki Ardhi; Haki ya kupata Huduma za Kibenki bila ya vikwazo vya Vitambusho(NIDA au Passport ya TZ); Haki ya kupiga kura, kugombea na kuchaguliwa nafasi za Uongozi; Uwepo wa Sera ya Taifa ya Usimamizi na Uratibu wa masuala ya Diaspora; Haki ya kupata faida za Hifadhi za Jamii; Haki ya Kufanya kazi nchini TZ ktk Taasisi za Serikali; Haki ya Kuwekeza kwa Viwango sawa na raia wa TZ waliopo nyumbani; Haja ya kuwa na Mfumo rasmi wa Kitanzania wa kutuma fedha kutoka nje; Haki ya Kuasili Watoto (Adoption Right) na Haki ya Kupata Misamaha ya Kodi wakati tunapotuma TZ misaada yenye maslahi kwa taarifa kama Vifaa vya Hospitali, Madawa nk.
Ili hayo yote au baadhi yake yawe granted, Serikali ilihitaji kuangalia namna utekelezaji wake utakavyokuwa chini ya Hadhi Maalum, na namna ya kuya harmonize na Sheria zilizopo sasa, ili kwa kufanya hivyo, Serikali hiyo hiyo isije ikavunja Sheria. Sasa kazi inayofanyika, ambayo wengi wanaona inachukua muda mrefu, ni kuweka sawa mapendekezo yetu kwa Serikali ili iweze ku grant, at least by 100 or less percents, yale tuliyoyaomba.
Nevertheless, one may ask if Special Status is real.! Jibu ni kuwa, It is real and will benefit both the Government and Diaspora themselves by enhancing our involvement in national development and thereby increase remittances; Diaspora Investments and so forth.
Vile vile, tukumbuke: Mhe. Kiongozi wetu Mkuu na mpendwa alitutangazia alipokuja US mwezi Aprili, 2022 kwamba HM inaandaliwa. Aidha, Foreign Minister pia aliueleza Umma wa Diaspora na Waheshimiwa Wabunge wakati akiwasilisha Bajeti yake Bungeni mwezi Aprili, 2022 kwamba mapendekezo ya Hadhi Maalum yanaendelea kushughulikiwa na yatakamilishwa. Sasa mashaka yetu yanatokana na nini? Ni nyumba ya aina gani inayoezekwa bila Msingi na Kuta za kushikiria dari na paa kukamilika? Nadhani, hatuna sababu ya kutilia mashaka dhamira ya Serikali kutupa HM.
Binafsi ninaliona ni suala la muhimu na nyeti linalohitaji kuandaliwa kwa umakini mkubwa ili litakapoanza lisiwe na dosari. Nashauri tuendelee kuiamini Serikali yetu. Natambua, laiti isingetaka kutu -grant HM, ingekaa kimya na bado tusingepata.
Mbona huko nyuma hatukuwahi kupata ahadi ya aina hii? Tulimlaumu nani? Au tunataka kuiambia Serikali ilikosea kututamkia dhamira yake kutupa HM? Nashauri haikukosea kutushirikisha, ili sote tufahamu. Ndio good governance, ndio transparency inayosisitizwa hata huku Ulaya na Marekani.
Naomba tuwe wastahimilivu kidogo maana Hadhi Maalum will transform Tanzania Diaspora and our contribution katika maendeleo yetu binafsi na maendeleo ya Taifa letu. Asanteni.
Admin.