
ITALY – ZANZIBAR BUSINESS AND INVESTIMENT FORUM
Na Mwandishi wetu
Zanzibar
WU Media PRODUCTION LIMITED
Kongamano kubwa la kibiashara Kati ya Italy na Tanzania limefanyika Leo Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kwanza ambapo itafuatiwa na kongamano la pili litakalofanyika siku ya kesho Jijini Dar Es Salaam.
Kongamano hilo ambalo lililofunguliwa na Makamu wa kwanza wa Rais Mh. Othman Masoud ambae alimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Hussein Mwinyi, limemalizika kwa mafanikio makubwa.
Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania Mh Marco Lombardi, walipata fursa ya kuongea na wadau wa biashara wa Italy na Tanzania. Katika kuhimiza Diplomasia ya Uchumi, Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo aliwataka wadau wa biashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za kibiashara hasa za masoko ya bidhaa za KILIMO kama Parachichi nk.
















