
Anaandika Dr Yahya Msangi
WU® MEDIA
“USHINDI WA GIORGIA MELONI NI FURSA KWA AFRICA”
Ushindi WA Binti WA kitaliano unapaswa kutufikirisha tena kuhusu Suala la LGBTIQ+.

Kwanza nisahihishe dhana potofu. WENGI huliita swala hili “ndoa ya jinsia moja” Lakini ni suala pana zaidi ya kuoana jinsia moja. Kuoana jinsia Moja ni sehemu Ndogo tu ya Suala hili.
Dhana hii inavipengele vingi ikiwemo mpaka kujamiiana au kuona mzazi na mtoto, ndugu kwa ndugu, binadamu na mnyama, uongozi wa kidini, kisiasa, mitaala ya elimu, michezo, n.k. Kudhani ni ndoa ya jinsi moja ni kutoijua hii dhana. Na usipoielewa hii dhana na mawanda yake hutaweza kuikabili vyema. Herufi pamoja na hiyo Alana ya kujumlisha (+) zina maana yake!
Kwa mfano yapo mapendekezo ya kuzingatia ushiriki wa LGBTIQs persons kwenye Olympic, word cup, para olympic, winter Olympics, boxing, NBA, EUFA, n.k. Yapo mapendekezo ya kutenga viti Maalum kwenye mabunge kwa LGBTIQs+ constituencies (majimbo ya LGBTIQs+).
Kwa nini nasema ushindi wa binti Italy ni Fursa?
Binti huyu Katangaza waziwazi hataki kusikia Habari za LGBTIQs+ katika utawala wake. Ameapa hatawaongezea haki yôyote zaidi ya ambazo tayari wanazo kisheria. Na anaapa kama sio sheria angezifutilia mbali na kutangaza ni uhalifu kuwa kundi la LGBTIQs+.
Binti huyu kaongeza kuwa hatakubali raia wa Italy wateseke kwa vita ya Ukraine isiyowahusu. Anasema atashirikiana na Putin kuhakikisha raia hawakosi gesi.
Macron wa France amejitokeza waziwazi na kudai dada hana AKILI . Eti LGBTQIs+ ni haki ya binadamu na kwamba Lazima NCHi za EU zimpinge Putin kwa pamoja.
Dada hakumkawiza. Katia hotuba iliyomwacha Macron na France uchi. Dada amemweleza kuwa Ufaransa Ndiyo chanzo cha maovu haswa dhidi ya waafrika. Waafrika wanakimbilia ULAYA kwa kuwa Ufaransa inaiba kwa Nguvu uranium Yao, ilishiriki kuiangamiza Libya, inahodhi fedha kupitia Faranga. Inawatoza waafrika tozo kwa kuchapisha Faranga. Yaani waafrika wanalipa tozo ya kuchapishiwa héla Yao. Na akurudia kumwambia LGBTIQs+ ni dhambi na hayuko tayari kuhalalisha dhambi hii katika nchi iliyo n’a makao makuu ya kanisa Katoliki!
Ungetegemea usikie viongozi wa kiafrika wakimuunga mkono dada huyu! Nadhani hâta yéyé anatushangaa ukimya wetu waafrika!
SERIKALI za kiafrika zinapaswa kuweka mkakati maalumu kukabiliana na janga la LGBTIQs+. Tusipoweka mkakati watashinda tupende tusipende. Tizama Cuba? Imesalimu amri sasa imekuwa halali!
Hela iliyowekezwa ni kubwa mno. Kuna taasisi nyingi mnoo zenye kumwaga fedha.
EU wana programme ya Human Right inatoa MPAKA euro milioni 5 kwa taasisi itakayo promote LGBTIQs+! Ipo taasisi ya anayejiita “shangaziiiii” ilipata fedha Hizi MIAKA kama 4 iliyopita. Ndiyo unaona anafanya vurugu. Anahalalisha matumizi! Zipo taasisi kama MAMA CASH, ROMEO & JULIO, CLEOPATRA, RAINBOW, KAMA SUTRA n.k. zimejipenyeza. Hâta Tanzania zipo. Tena Tanzania imepewa priority mara tu baada ya Marie Stops kupigwa stop, Amba kushitaki, Makonda kutangaza atawakamata na Akaunti kufuatiliwa. Tanzania imewekwa orodha ya highly targeted countries.
Tunapaswa kuzitambua Hizi taasisi, kuzipiga marufuku zisi operate nchini, kukamata fedha wanazotoa kwa vi NGO vyetu, kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaopokea fedha kwa ajili ya ku promote LGBTIQs+ , kuzifutia usajili, n.k. Tuwe wakali la sivyo Iko Siku utaenda Msaada bungeni kuruhisi huu ujinga. Msidhani wapambe hawapo bungeni. Wapo! Kama wanatoa hoja tuhalalishe bangi watashindwaje kudai kila mtu aachwe aamue mwenyewe kuolewa na babaake au kumuoa mamaake? Kama MTU anaweza kulipa nauli Kwenda kudai watoe wa shule kupata mimba ni haki itashindikana kudai akiwa mlawiti wenzake aachwe aendelee kusoma na kulala bweni na wénzake?
Hata humu Facebook wamo subiri utawasikia.
Nchi za ghuba ndivyo wameweza kuzuia. Kina Romeo & Juliet wamehangaika weee imeshindikana kuhalalisha.
Tumuunge mkono huyu dada wa Italy japo sidhani atadumu maana kawagusa wenye héla. Watafanya juu chini serikali yake ianguke haraka. Lakini katusaidia mawazo.
Vita hii tukiiacha hivi tutashindwa! Tutashuhudia ndoa za mama na mwana, baba na binti, kaka kwa kaka. It’s just a matter of time.