
Italy – Tanzania Business and Investment Forum
WU® MEDIAPRODUCTION LIMITED
Na Mwandishi wetu, Dar Es Salaam
Waziri mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Mulamula amepongeza uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Italy na kuzitaka sekta za uwekezaji nchini Tanzania na Italy kufanya kazi kwa karibu kwa manufaa ya nchi.
Hayo yamesemwa katika hafla ya kufunga Kongamano la pili la Biashara kati ya Tanzania na Italy katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar Es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahamoud Thabit Kombo na Balozi mwenzie Mh. Marco Lombardi , Balozi wa Italy nchini Tanzania, wamekuwa na ushirikiano mkubwa katika masuala ya kidiplomasia na Zaidi kwenye Diplomasia ya Uchumi.


