Na Dr Yahya Msangi
Mikutano WA 27 (COP 27) wa UN utaanza tarehe 6 hadi 18 November kwenye kisiwa cha maraha pembezoni na bahari ya Mediterranean. Dunia itaendelea kujadili namna ya kukabiliana na mabadiliko tabia nchi. Viongozi na wataalamu mbalimbali watahudhiria. Nadhani mimi ni mmoja wa binadamu wachache waliohudhuria kuanzia COP 1 hadi COP 27. Yaani miaka 27 na ushee.
“Kwa mantiki hii ushauri wangu ni wa kuzingatiwa kama héla.“
Nimeona mengi kwenye huu mjadala. Nilikuwepo walipokubaliana Paris Agreement 2015. Niliona Trump alivyokataa.
Nimeona jinsi waafrika wanavyokuja bila kujiandaa na wanavyogonganishwa. Nimeona misafara ya waafrika ilivyo na mapungufu. Wachache, wanachaguana bila kuzingatiwa ujuzi, hawakai ukumbini haswa usiku, wanaunga mkono hoja za kuwauliza bila kujua, n.k.
Ikifika mada ya héla Ndiyo utawaona walivyoshupaa!
Leo Ningependa kuongelea jambo Moja ambalo sijawahi kusikia Nchi yôyote ya Afrika au AU wakiidai kwa takriban miaka 27 ya majadiliano.
Issue yenyewe ni nishati ya nyuklia. Nuclear Energy!
Najua hâta wasomaji baada ya kusikia nuklia mnatishika. Wenzetu wamesambaza Uongo na uoga Ili waendelee kutudumaza. Waafrika tumeaminishwa kuwa nishati ya nuklia ni hatari. Eti hatuiwezi. Tumeelekezwa kwenye Solar, Maji( hydro), biogas, upepo (wind power) na nishati zinazoitwa “endelevu” ili tuendelee kuwa masikini. Utasikia Sisi wenyewe tukiambiana “waafrika wazembe tutaangamia”! Au darasani kikifika kipindi cha nuclear science tunaenda kula mahindi ya kuchoma. Tunaamini hatuwezi kuelewa.
Ningependa katika COP 27 NCHI za kiafrika zianze kufikiria kujenga kituo kikubwa cha umeme wa nuklia (Africa Nuclear Energy Plant). Kimoja tu ! Kitatosha kusambaza umeme wa uhakika kila nyumba, mtaa, Kijiji, mji Afrika!
Bila umeme wa nuklia hâta tujenge mabwawa 1000 kama la Stiegler tutaendelea kukaa gizani kama kombamwiko. Tutaendelea kubishana kuhusu uharibifu wa mazingira ya vyura!
Afrika kwa pamoja inaweza kuijenga kinu cha kufua umeme wa nuklia na wakauza umeme Nje.
Wakati umefika sasa wa kuacha kuogopa umeme wa nyuklia. Umefika wakati tuamke !
Makala ijayo nitaeleza ni kwa Nini tunaonekana Wajinga kuhusu suala hili. Ni kwa nini wazungu wanatuelekeza kwenye mabwawa ya Maji, solar, upepo, biogas, n.k.
Ni kwa nini tuna NGOs na wanaharakati uchwara wanaotumika kupinga nishati ya nyuklia.
Inshaallah.
Kwa sasa ngoja nilambe asali Charm El Sheikh! Kwa Gamal Abdul Nasser