
Washington DC WU® MEDIA
MREJESHO WA MKUTANO WA VIONGOZI WA JUMUIYA ZA WATANZANIA USA NA MHESHIMIWA BALOZI JAMES MBWANA AMBAE NI MKURUGENZI WA DIASPORA WIZARA YA MAMBO YA NJE WASHINGTON DC. OKTOBA 29, 2022
Katika maombi yote yaliyowasilishwa na Diaspora kuhusu hadhi maalumu, mambo yafuatayo ndiyo yaliopitishwa.
- Fursa ya kuingia Tanzania, kukaa na kutoka bila ukomo wala kulipa visa.
- Haki ya kurithi na kurithisha ardhi.
- Kuadopt watoto Tanzania.
- Kupata huduma zote za kijamii (Kufungua akaunti za benki kama watanzania).
- Kupata msamaha wa kodi kama Watanzania.
- Kuwekeza kwa masharti bila masharti ya mtaji kama watanzania wengine
- Kushiriki katika mifuko ya jamii (NSSF nk).
- Kuweza kujiunga na Bima za afya na kuwawezesha wanafamilia Tanzania kuwa katika mpango huu.
- Consultants Diaspora wa Tanzania watapewa Fursa kwanza kabla ya Wageni.
- Wana diaspora wanaotaka kufanya kazi za kujitolea wakiwa Tanzania hawatatozwa malipo yoyote kupata vibali rasmi.
● Haki hizi zitatambulika kisheria kwa mfumo wa kadi maalumu.
● Kadi hii itakuwa na muda maalum (Miaka kati ya 5 au 10) na italazimika kurenew kama passpoti. Kurenew hakuathili hadhi yako.
● Kadi hizi zitatolewa kwa vizazi vyote vyenye nasaba ya UTANZANIA (Watoto, Wajukuu, Vitukuu nk).
● Kutaanzishwa utaratibu wa kidigitali wa kujiandikisha wanadiaspora wote duniani ili
kupata idadi kamili ya wanadiaspora ili kurahishisha zoezi la utayarishaji wa
vitambulisho hivi.
● Mfumo huu wa kidigital utawezesha DIASPORA kupata huduma zote muhimu (NIDA,
MABENKI, BIASHARA nk)
● Vitambulisho vya NIDA vitaanza kutolewa (Pilot program) katika balozi za Tanzania nchini USA, UK na CHINA kuanzia Dec 2022 Kwa wale Wenye sifa.
FARAJA KWA WALIOJILIPUA
Usiku ukikomaa, karibu kupambazuka!
Serikali inatambua kuwa kuna waliojilipua. Hivyo katika mchakato wa kutoa Hadhi Maalumu, serikali itataka ipate tu uthibitisho wao wa kuwa wao ni wazawa wa Tanzania bila ya kujali paspoti zao za ukimbizi zinaonyesha wamezaliwa wapi.
Hii ni faida kubwa sana kwa waliojilipua. Kwa sababu kama ingekuwa ni uraia pacha paspoti zao za nje zingeonyesha wamezaliwa Somalia, Congo, Burundi nk, wakati paspoti zao za Tanzania zingeonyesha wamezaliwa Tanzania.
Kwa maana nyingine wasingeweza kuzionyesha hizo paspoti mbili kwa pamoja bila ya kupata matatizo ya kisheria ambayo yangepelekea kufutiwa uraia wao wa nje.
