0 0
Read Time:1 Minute, 38 Second

WU® MEDIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ili Taifa liweze kupata mafanikio ,kunahitajika uwepo wa vipaumbele na shabaha zinazoweza kupimika ,sambamba na mipango iliyo makini na ufuatiliaji.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika uzinduzi wa Taasisi ya Afisi ya Rais ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB) halfa iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Amesema mafanikio yanahitajika kuwepo kwa vipaumbele ,mipango making ya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuweza kutatua matatizo yanayojitokeza na kuepuka ucheleweshaji.

Alisema jukumu kubwa la PDB ni kuhakikisha kunakuwepo Utekelezaji wa vipaumbele vilivyoainishwa kwa wakati unaofaa.

Rais Dk.Mwinyi amesema kwa kuanzia utekelezaji vipaumbele hivyo utahusisha sekta nne za Miundombinu,Utalii ,
Maendeleo ya kijamii pamoja na Uchumi wa Buluu.

Rais Dk.Mwinyi alieleza kuwa PDB ni kitengo maalum kilicho chini ya Ofisi yake,kinachoundwa na timu ya wataalamu walioajiriwa kwa utaratibu wa ushindani na uwazi.

Alisema taasisi hiyo itaondoa vikwazo,kubaini uhaba wa rasilimali na masuala mengine yanayoweza kuchelewesha maendeleo,ili kufanikisha lengo la Utekelezaji wa ahadi zake kwa Wananchi.

Aliwataka Viongozi na watendaji Serikalini kubadilisha na kuharakisha njia za kufanyia kazi kwa kuondokana na utendaji wa mazoea.

Aidha,alisema ili kufikia mafanikio,Taifa linapaswa kujifunza kutoka kwa wengine na kukubali usaidizi kutoka kwa wahisani na marafiki ,kama vile Taasisi ya Tony Blair (TBI) na Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP,huku mkazo ukiwekwa katika kuwajengea uwezo watendaji Serikalini.

Alitoa wito kwa wananchi wote wa Zanzibar kushirikiana na Taasisi hiyo ,huku kila mmoja akiwajibika kwa nafasi yake.

Rais Dk.Mwinyi ametoa pongezi kwa Taasisi ya Tony Blair(TBI),Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP pamoja na timu nzima ya Watendaji wa PDB kwa kufanikisha uanzishaji wa taasisi hiyo .

Halfa hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa kitaifa,kimataifa wakiwemo Mawaziri,Makatibu wakuu ,Mabalozi ,Washirika wa Maendeleo,Wakuu wa Mikoa ,Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Dini.

02 Disemba 2022.
Ikulu,Zanzibar.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %