25 – 27 January 2023 , DAKAR SENEGAL

MKALI AMPONGEZA MWANDISHI LAISER.
Ndugu Laiser,
Ahsante kwa mchango huu maridhawa sana.
Kwa nyongeza: (1) Ni asilimia 60 (60%) ya ardhi ya kilimo duniani ipo Afrika. Hivyo basi, ni zaidi ya aibu, Afrika kuwa omba omba wa chakula. Hii ni fedheha.
Aidha katika mikakati ya kukuza kilimo barani Afrika, kilimo cha uhandisi jeni (GMO) ni lazima kiwe out of the equation. GMO ni silaha katika vita vya kufuta kujitegemea kwa wakulima duniani.
(2) Miaka ya 1960s Afrika ilikuwa inazalisha asilimia 7 ya chakula cha ziada.
(3) Baada ya kuletewa “Structural Adjustment Programmes (SAPs)” zilizolazimisha Afrika kufuta ruzuku kwa wakulima, kufuta elimu bure na afya bure kwa wananchi wetu ili tuweze kulipa madeni yao ya kitapeli, ndipo ile asilimia 7 ya chakula cha ziada iligeuka kuwa asilimia 11 ya “food deficit.”
(4) Wakati wanalazimisha Afrika kufuta ruzuku kwa Wakulima wake, asilimia zaidi ya 50 ya bajeti ya Umoja wa Ulaya ilikuwa ruzuku (si mkopo) kwa wakulima wao. Kama kuwanyima “subsidies” wakulima ni sera nzuri kulikoni wao wenyewe walikuwa hawaifuati hiyo sera?
Hivyo basi ni muhimu sana Viongozi wa Afrika kujikumbusha wapi tulijikwaa, vinginevyo hii mikutano itaendelea kuwa ni bure ghali.
Ahsante ndugu yangu , nimeipenda sana makala yako.
mkali@live.co.uk
11/01/2023.








