
MIAKA SABA NA HOJA 1000 ZA WAPINZANI WA MAMA SAMIA.
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Januari 13,2023.
Vyama vya Upinzani NCHINI vimejigamba kuwa na kapu la hoja 1000 ndani ya miaka saba ambayo walikuwa “kifunguni” na wameanza kutisha CCM kuwa pindi watakapoanza mikutano ya hadhara basi Nchi itatikisika”Political Mind Game”.
Gazeti la Raia Mwema la Januari 11,2023 lilibeba kichwa cha habari hiki “NGOMA NZITO”, huku likiwa na sub-heading 3 “wapinzani na hoja 1000 za miaka saba,Chadema kutumia Ruzuku kuzunguka na Chopa na Tundu Lissu na Lema kurejea kuongeza nguvu”.
Kitu ambacho wanafanya kwa sasa Wapinzani sio kigeni kwenye Siasa za sasa!Wapinzani wanajaribu kutaka “kuwajaza upepo” wana CCM kwa lengo la kuwavuruga kabla ya kuanza kwa mikutano ya hadhara baadae mwezi huu!”Political Mind Game”.
I.HOJA 1000 NDANI YA MIAKA SABA YA KIFUNGO!
Hoja 1000 za wapinzani ndani ya kile walichokiita kifungo cha miaka saba zinaweza zikawa zimemezwa na miaka saba ya kazi kubwa ya CCM katika kuwaletea watanzania maendeleo!CCM inaweza ikawa na majibu 10,000 dhidi ya hoja 1000 za miaka saba za wapinzani!
Miaka saba ya Serikali ya awamu ya tano na Serikali ya awamu ya Sita inabeba image ya CCM kuwa na ushawishi mkubwa zaidi labda kuliko kipindi chochote hasa kwa Vijana wakina Mama na Wazee ndani ya miaka 27.
Miaka saba ya hayati JPM na Mama Samia Suluhu Hassan ilibeba maajabu makubwa ya miradi ya maendeleo kwa Watanzania kuliko wakati wowote katika historia ya Tanzania!Bwawa la Umeme la Nyerere,SGR,Makao Makuu kuamia Dodoma,Flyovers,ununuzi wa madege na zaidi uwajibikaji wa Serikali kwa Wananchi!
Kwa kifupi,wapinzani watakuwa wanaibeba sana CCM wakija na hoja zao 1000 kwani zinaenda kuwafanya wana CCM ambao ni “wavivu” kusema mafanikio yao kwenda sasa kuyasema kwa Wananchi hivyo kuwafanya kuweza kukubalika zaidi!
Automatically hoja 1000 za miaka saba zinajibiwa na kazi kubwa ya CCM ndani ya miaka saba ya awamu ya tano na awamu ya Sita!
II.CHADEMA KUTUMIA RUZUKU KUZUNGUKA NA CHOPA!
Chadema bado wanaendelea na makosa yale yale ya 2020 ya kutaka kuwafikia watu kwa CHOPA!Chadema walipaswa kwanza kuanza na kitu kinaitwa “Political installation” kwanza baada ya kupotea kwa miaka karibia saba!
Political recruitment could be better zaidi kama ambavyo walifanya huko nyuma katika kuwapata wakina Ernest Silinde,John Mrema na vijana wengine na kuweza “kuwainject” falsafa mpya KUELEKEA 2025.
Kila siku nasema Chadema wanakosa “Think Tank” na Political Strategists wa maana!CDM ni kama wamekumbwa na “barehe” ya kutaka kuanza kufanya Siasa kumbe walipaswa kuwa strategic zaidi kwa kufanya kitu kinaitwa kwanza “Political re-orientation”.
Hauwezi kukamata dola kwa “barehe za kisiasa” kama hizi!CDM wanahitaji muda wa kufanya kitu kinaitwa (i) Appreciation of the situation” kwanza kabla ya “kujideploy” kwenye mikutano ya hadhara!Business as usual,hauwezi kuishinda CCM ya Kanali Kinana kwa style hiyo,hauwezi!
III.TUNDU LISSU LEMA KUREJEA KUONGEZA NGUVU!
Ushindi Vitani unategemea mambo mengi lakini moja la msingi ni “selection and maintainance of the aim”.Swali Je, mikutano ya hadhara ya wapinzani ina political target ipi?
Je(i) kufanya Political re-recruitment?(ii)kueleka kutaka kuchukua dola 2024 + 2025?(iii)re-branding?
Je ,Chadema wamejibu maswali ya Mikutano ya hadhara for what,for who,when and how?Je,Wapinzani wana mpango kazi mkononi wa kuelekea Mwaka 2025 na ikibidi Mwaka 2030?,Je,wanao mpango kazi huo huo?,au wanarush tu kwenye mikutano ya hadhara!
Itakuwa ni ndoto za mchana kupambana na CCM ya Mh. Samia Suluhu HASSAN Mwaka 2025 kama wapinzani wenyewe ndio hawa!Wait & See!
+255746726484.





Kazi yenu ni njema
asante sana mkuu