MIAKA MIWILI YA RAIS MAMA SAMIA YAANZA”KUWATISHA” MAJIRANI ZAKE.
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
January 16,2023.
Nchi za Kenya,Uganda,Burundi,DRC na Rwanda zimeanza kutishwa na spidi ya kukua kwa Uchumi wa Tanzania kwa maana ya “GDP” chini ya Serikali ya awamu ya Sita ya Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka karibu miwili pekee yake!
Hofu hiyo imetangazwa rasmi na Maofisa wa Serikali ya Kenya kupitia kipindi maalum cha Luninga kupitia Televisheni yenye Ufuasi mkubwa Nchini Kenya yaani Citizen TV,hivi karibuni.
Hii ni habari njema kwa Chama cha Mapinduzi na Serikali ya CCM ya awamu ya Sita kwani huu ni “unabii” kutoka nje ya mipaka ya Nchi ya Tanzania kutoka ndani ya vyanzo vya Serikali ya Kenya yenyewe! Hauwezi kuita Propaganda hata robo!
Uoga huo unakuja baada ya GDP ya Tanzania kuonekana kukua kwa kasi ya kutisha ndani ya Serikali awamu ya Sita na Serikali ya awamu ya tano ndani ya miaka sita pekee yake!,vyanzo vya habari kutoka Citizen TV ya Nchini Kenya vimeweka wazi “uoga” huo hivi karibuni!
GDP ya Tanzania Mwaka 2015 ilikuwa ni 47 USD Bilioni pekee wakati Nchi ya Kenya Mwaka 2015 ilikuwa na GDP ya 80+ USD Bilioni karibia mara mbili ya Nchi ya Tanzania!
Mwaka 2022 GDP ya Nchi ya Kenya ni 110.4 USD Bilioni wakati kwa takwimu za Mwaka 2022,GDP ya Nchi ya Tanzania ilikuwa inasoma 76 USD Bilioni.Mama hatari sana!
Takwimu za hivi karibuni zinatabiri GDP ya Tanzania kwa Mwaka 2027 Miaka Mitano tu kuanzia sasa itakuwa 120 USD Bilioni ongezeko la Bilioni 40+ USD.Hatari sana!Mama anaenda kuset history ya pekee kuelekea ukomo wake Mwaka 2030!
” …tough time ahead”,ilikuwa moja ya nukuu ya Citizen TV ya Kenya katika kipindi hicho cha hivi karibuni!
Wakenya wanakiri kuwa kwa sasa, ulali wa biashara kati ya Tanzania na Kenya kwa kwa sasa upo upande wa Tanzania kinyume na Miaka ya 2015 kurudi nyuma na “wanacite” mpaka wa Namanga kuwa tayari kwa sasa umetekwa na Nchi ya Tanzania kibiashara “Export Maneuver”!
Hizi sio habari njema sana kwa wapinzania Nchini Tanzania kuelekea ufunguzi wa Mikutano ya hadhara hivi karibuni kwani “uoga” huu wa Wakenya unaipa “jeuri” Serikali ya awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan kwamba bado ipo kwenye “truck”.
Pia habari hizi zinashusha sana “confidence” ya wapinzani ambao tayari walijitapa kuwa na hoja zaidi ya 1000 za kuishambulia Serikali!Mpaka hapa “game” inaweza kuwa imegeukia kwao!
Si siri tena kuwa juhudi kubwa za Serikali ya awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan katika kutanua uwekezaji na kuongeza export zinaenda “kuivuruga” kabisa Nchi ya Kenya pamoja na majirani wengine!
Bandari ya Dar inatajwa kuteka biashara yote ya Bandari ya Mombasa baada ya maboresho makubwa lakini zaidi miradi ya kimkakati pindi utakapoanza kufanya kazi inaweza kuifanya GDP ya Tanzania “kuogopwa” zaidi sio tu ndani ya Ukanda wa EAC bali pia kwenye Ukanda wa SADC.
Miradi ya SGR,Bwawa la Nyerere,Mradi wa LNG,Mradi wa Madini wa Kabanga Nickel,Mradi wa Madini ya Dhahabu wa Nyanzaga Mkoani Mwanza na Miradi mingine mingi kwenye Sekta ya Ujenzi wa barabara Nchi nzima uenda ukaifikisha Tanzania kwenye Uchumi wa GDP ya 150 USD Bilioni kabla ya mwaka 2030.
Jukumu kubwa la Serikali ya awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan itakuwa ni jinsi ya kusimamia vizuri Uchumi huu uweze kufika kwa Watanzania wa chini kabisa Mikoani na Wilayani.
Na hapo ndio Mama Samia Suluhu Hassan anahitaji Umakini na Weledi mkubwa katika kuwaleta watu kwenye halmashauri zetu ambao wataweza kuendana na kasi ya Ukuaji wa Uchumi wetu na utatuzi wa changamoto za watu wetu huko vijijini na mijini!
Mpaka dakika hizi hapa,sioni hoja nzito ambayo inaweza kumzuia Mama Samia Suluhu Hassan kurudi Ikulu Mwaka 2025.
+255746726484.