
Na Mwandishi wetu
Johannesburg
Habari za kutatanisha na sintofahamu kubwa nchini Afrika ya Kusini kuhusu kifo Cha mtu aliyetambulika na Watanzania kuwa ni Raia wa Tanzania aliyekuwa akiishi nchini humo. Mtanzania huyo mkazi wa Johannesburg maarufu kwa jina la Abdi Sugu, alikuwa akiishi maeneo ya Fox Street Johannesburg. Kwa mujibu wa mashuhuda ni kuwa marehemu amefikwa na umauti siku ya tarehe 15/1/2023 akiwa mikononi mwa police baada ya kuvamiwa akiwa anarejea nyumbani kwake. Watanzania wamefanya maandamano kupinga mauwaji hayo na kusisitiza sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wahusika.
Bado chanzo halisi Cha tukio Hilo la kusikitisha hakija fahamika.
