0 0
Read Time:47 Second

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania GREECE amshukuru Balozi wa TANZANIA Rome

Athens Greece

Watanzania nchini Greece wamepata fursa ya huduma ya passport iliyotolewa na maafisa wa uhamiaji wakiongozana na maofisa wahusika wa ubalozi wa Tanzania Rome ambao ndio unaowakilisha nchi kadhaa za Ulaya na Balkan
Zoezi lilianza Jana tarehe 19/1 /2023, Maofisa wa Uhamiaji wakiongozana na Bw. Nnembuka kutoka ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy.Zoezi limefanyika mjini Athens kwanye ukumbi wa ofisi ya TANICA inayomilikiwa na familia ya Penessis (diaspora toka Bukoba)
Huduma hii tulikuwa tukiisubiri miaka mingi, na isingefanikiwa bila jitihada za hali ya juu alizozifanya balozi wetu Mh.Mahmoud Thabit Kombo. Kwa niaba ya Jumuiya ,napenda kumshukuru Mh.balozi.Aidha tunamshukuru bw. Nnembuka na wahusika wote wa Uhamiaji waliokuja kutuhudumia” amesema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania GREECE Ndugu Kayu Ligopora wakati akiongea kwa njia ya mtandao na Wabongo ughaibuni Media WU®

Diaspora GREECE wakipatiwa huduma ya passport
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %