
Shula’s kitchen
Na Mwandishi wetu
Antwerpen Belgium 28/01/2023
Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ukiwakilishwa na ndugu Anthony S.Mtafya (HOC) ambae pia ameongozana na Bi Vivian A.Rutaihwa na Ndugu Juma Salum ambae ni msimamizi wa dawati la diaspora Ubalozi wa Tanzania Belgium. wamehudhuria sherehe ya ufunguzi wa Restaurant ya Mtanzania (DIASPORA) anaeishi mjini Antwerpen
Katika ghafla hiyo pia ilikuwa na bahati ya pekee kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo alieongozana na Mkewe.
Katika hafla hiyo walishiriki Wana diaspora kutoka nchini Belgium na Luxembourg ambako pia ni eneo la uwakilishi wa ubalozi wa Tanzania Belgium
Mwenyekiti wa Diaspora nchini Ubelgiji Ndugu Riziki Thomas wakati akiongea na WABONGO UGHAIBUNI MEDIA kwa njia ya mtandao alisema “Ubalozi wa Tanzania nchini Belgium pamoja na majukumu makubwa ya uwakilishi wa Nchi yetu lakini wamekuwa karibu na Diaspora kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Jumuiya ya Watanzania kuwaunganisha Watanzania, kushirikiana katika kuleta Maendeleo kwa Watanzania nchini Belgium ili waweze kuzitumia fursa za uwekezaji nyumbani Tanzania, na kwa kufanya hivyo kutaweza kuchangia Maendeleo.“
Shula’s kitchen ni restaurant ambayo itawafanya Watanzania na watu wa East Africa kujisikia wako nyumbani kwani Dada Ashura ni mbobezi wa mahanjumati.









Picha na Lilian Nabora
Antwerpen Belgium









