
WU® MEDIA
Engine moja yazima
TAHARUKI!?
Habari ya Asubuhi Ndugu Zangu natumani ni wazima,
leo Wakati tunasafiri kutokea Dar kwenda Dodoma kutumia ndege ya Precission PW 600, kuna jambo limetokea,
tupo hewani nilikuwa nimekaa dirishani, wakati tunakaribia kushuka Dodoma nikaona engine imezima, tupo hewani OMG…Rubani akatangaza kurudi Dar kwa dharula kwa kutumia Engine Moja, ndege ikageuza kurudi Dar kwa kutumia Engine Moja, hali ilikuwa mbaya Sana Ndani ya ndege but tunamshukulu Rubani kwa kutushusha Salama.
Naomba Mamlaka husika zinazoshughulikia Maswala ya Anga (Aviation) kuhakikisha hizi ndege zinafanyiwa Services ya kutosha kwani wanaweka rehani Maisha ya watu wengi Sana, tunamshukulu sana Mungu ametupigania kwani bila yeye Mambo yangekuwa tofauti kabisa.

Joseph Rwegasira Samson
Deputy Mayor – Kinondoni Municipal Council
