
Na Mwandishi wetu
Rome, Italy

Waziri wa Mifugo na Uvuvi

Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi,leo tarehe 30/03/2023 amekutana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Italia, Waziri Ulega amekutana na kufanya Vikao na Mkurugenzi wa Africa Sig. Giussepe Mistretta, Mkurugenzi Benki ya Maendeleo ya Nchini Italia Sig. Mucci pamoja na Mfuko wa Maendeleo wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia SACE na CDP.
Rome
Katika vikao hivyo Mh. Waziri ameongozana na Ujumbe wake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Pamoja na Ujumbe wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia ambao ulioongozwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mahmoud Thabit Kombo .


Ziara hiyo imezaa mafanikio makubwa kwa makubaliano ya kuanza kazi katika maeneo mbali mbali ya Mifugo kupitia Ranchi za Serikali zilizopo chini ya Kampuni ya Serikali ya NARCO, Machinjio ya Kisasa na Miradi mbali mbali katika Sekta ya Uchumi wa Buluu ambao Serikali ya Italia ilishatenga fungu Maalum la fedha kwa ajili ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Mhe. Waziri Ulega pia aligusia maeneo maalumu ya mashirikiano na uwekezaji kupitia mifuko hiyo ambapo maombi hayo yalipokelewa na yanaanza kufanyiwa kazi mara moja.
Itakumbukwa kuwa Mhe. Ulega ana mwezi mmoja tokea ateuliwe kushika wadhifa huo ambapo ameanza na Kasi ya Vitendo kwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uvuvi na Wavuvi wadogo wadogo kupitia Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO. Kesho Mh Waziri anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano huo wa Ulimwengu mzima katika masuala ya Uvuvi. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inategemewa kufanya mawasilisho maalumu kuelezea mafanikio na changamoto mbali mbali katika Sekta hiyo ya Uvuvi.


