London UK, 24-04-2023
Pembezoni mwa Mkutano wa UK-Africa Health Summit, Wizara ya Afya Zanzibar imesaini makubaliano na Barking, Havering and Redbridge University Hospitals ya ushirikiano katika sekta ya afya.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania UK, Dr Migiro amepongeza mchango wa TUHEDA uliofanikisha makubaliano hayo. Tuheda ni Jumuiya ya Madaktari wa Watanzania wanaoishi na kufanyakazi nchini Uingereza.