WU® MEDIA
Watanzania 200 na baadhi ya Waafrika wa nchi nyingine waliokuwa Sudan wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kati ya saa 10 hadi 11 Alfajiri ya tarehe 27 April 2023.
Safari ya kurejea nyumbani ilianzia Khartoum Kwa mabasi, majira ya saa 7.30 mchana ya tarehe 24 April 2023 na kuelekea Mji wa Al Qadarif ambao upo takriban kilometer 420 kutoka Khartoum.
Msafara ulifika Al Qadarif usiku na kulazimika kulala kutokana na usalama na kuondoka asubuhi ya tarehe 25 April 2023 kulekea Mji wa Metema, Ethiopia ambao unapakana na Sudan. Metema Iko kilemet 161 kutoka Al Qadarif.
Kutoka Metema, Msafara ulianza safari kuelekea Mji wa Gondar, Ethiopia ambao uko kilometer 220.
Kutoka Gondar Watanzania hao 200 na raia 10 wa nchi nyingine za Afrika walisafiri Kwa ndege kwenda uwanja wa Bole, Addis Ababa.
Kutoka Addis Ababa wata chukuliwa na Ndege ya Tanzania (ATCL) dreamliner kuja Dar es Salaam.
Summary ya route:
- Kutembea Kwa miguu kutoka kwenye Makazi yao kwenda meeting point – International University of Africa (IUA), Khartoum huku mapigano yakiendelea (hatari tupu).
- Safari kutoka IUA-Khartoum kwenda Al Qadarif (420km) Kwa mabasi na kulala usiku mmoja
- Kubadilisha mabasi na kusafiri kutoka Al Qadarif hadi Metema mpakani Ethiopia (160km).
- Kusafiri Kwa mabasi tena kutoka Metema kwenda Gondar Airport, Ethiopia (220km).
- Kusafiri Kwa ndege kutoka Gondar kwenda Bole – Addis Ababa.
- Kusafiri Kwa ndege ATCL kutoka Bole Addis Ababa hadi Dar es Salaam.
Abiria wengi wa nchi nyingine watakabidhiwa Kwa Balozi zao Addis Ababa
Raia mmoja wa Uingereza mwenye asili ya Tanzania atasafiri hadi Dar es Salaam.