0 0
Read Time:2 Minute, 5 Second

Baada ya BONGOZOZO kutoa Kauli kuhusu sheria za TANZANIA zinazokataa uraia pacha na badala yake serikali inajipanga kutoa hadhi maalumu kwa Diaspora wa Tanzania na vizazi vyao, kumezuka majibu na mijadala kwenye makundi SOGOZI ya Diaspora.

Kutoka Makundi SOGOZI

H******: Yaani mmeamua kumponza baba wa watu aongee *** hizi?🤷‍♂️
Kwahiyo kumbe kesi yenu ni kupata uraia pacha na sio kutafsiriwa?

Taratibu mnajionyesha ni jinsi gani mlivyo wehu wa kudharau sheria za nchi yenu kwa tamaa ya kuwa na pass mbili yaani uraia pacha.
Huyu mzungu yeye uraia pacha utawasaidia nini wanawe kuliko hii hadhi maalumu ambayo itawatambua wanae kwa uzawa wao.

Watanzania wameanza kuingia ughaibuni kabla ya yeye kuzaa hao watoto na hakuna kilichopungua kwa nchi.
✓ Z*****: Watoto wake waliozaliwa Tanzania wana haki ya kuchukua Hadhi Maalumu Tanzania. Yeye kama abaki na benefit zake za Uingereza, kaziona mali kuliko Utanzania halafu anajiita mzalendo namba
mbili.

Na kama yeye ni mzalendo aelewe yeye sio mzungu pekee anayeitamani Tanzania, iko mibeberu kama alivyosema mwenyewe. Hatuwezi kuuza nchi kwa sababu ya Bongo zozo.

Huu ni mfano hai kwa wale mafala wa clubhouse wanaosema uraia pacha ukitolewa hakuna wazungu na wageni watakaochukua uraia Tanzania.

Bongo zozo amethibitisha ana vigezo vyote vya kupata uraia Tanzania sasa hivi. Kuoa mtanzania, ukazi wa muda mrefu, pengine na uwekezaji pia, lakini kuukana uraia wa Uingereza ndio kikwazo pekee kinachomfanya asichukue uraia Tanzania.

Wako wengi hawa, sio yeye peke yake.
✓H***** Kauli kama hizi zilipaswa kutolewa kabla serikali haijatoa maamuzi ya kutoa Hadhi Maalumu kwa watanzania Diaspora.
Lakini kwa sasa kuongea hivi huku ukijua ya kwamba serikali imeshatoa muelekeo wake basi tuseme kwa ufupi tu ni “Fujo isiyoumiza.”

Wanadiaspora nashauri tuwe waelewa na watu wa kusoma alama za nyakati.

Kwani kilio cha wanadiaspora miaka yote ya nyuma ilikuwa ni Uraia Pacha ambao taarifa ilifika serikalini kwa njia nyingi tofauti na hatimaye mwaka 2014 serikali ikatoa muono wake kuwa itatoa Hadhi Maalumu.

Kumbuka kuwa ni Serikali hii hii ndio iliyoimbwa na kuja na majibu ya HM.

Sasa kitendo cha kuendelea kupiga kelele za Uraia pacha kina maanisha nini kwa serikali ambayo inaandaa Hadhi Maalumu?

Tuna weza tukawa tunashangilia maneno matamu na kusahau kuwa kwa maana nyingine ni kwamba tunadharau kile ambacho tunatakiwa kupewa kwa kuanzia.

Tujifunze kukumbushana na kujulishana kuwa Serikali ni serikali na inaviongozi na watanzania ambao wameishi Ughaibuni na Wanawatoto ughaibuni lakini wameamua kuanza na Hadhi Maalumu.

Tusijione kuwa sisi ni wa muhimu sana na tunapaswa kupewa tunachotaka.

Lazima tutambue kuwa hata bila sisi nchi itaendelea na inaendelea bila vikwazo vyovyote.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %