
Tanzania
Popote utakapoenda duniani, Tanzania inabaki kuwa nyumbani.

Leo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imezindua rasmi mfumo wa kidijitali utakao kusanya na kutunza taarifa za Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora Digital Hub).
Mfumo huu utakuwa ni njia rahisi ya kupata taarifa sahihi za Watanzania walio nje ya nchi na kuwashirikisha katika masuala mbalimbali ya Kitaifa.
Kufanikisha utengenezaji wa mfumo huu, Benki yetu imedhamini kiasi cha
Shilingi Milioni 100 tukitambua namna mfumo huu utakavyosaidia sekta ya fedha na kuharakisha maendeleo nchini.
Sherehe za uzinduzi zimeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki – Dkt. Stergomena Tax na tumewakilishwa na Afisa Mkuu wetu wa Wateja Binafsi na Biashara – Filbert Mponzi.
Hatua muhimu sana hii kwa sababu Miongoni mwa changamoto za Diaspora wetu ni kujua idadi yao halisi huko waliko.