Na Mwandishi wetu “KL“
Athens, Greece
CEO wa Nala Money, Ndugu Benjamin Fernandez kwa mara ya kwanza akiwa na Timu yake Wamefanya utambulisho Rasmi wa Nala Money nchini Ugiriki.
Benjamin Fernandez na wasaidizi wake walikutana na viongozi wa Jumuiya ya Tanzania , Kenya, Uganda,Nigeria ,Senegal,Ghana,Gambia,Cote D’ivore na Cameroon.
Team ya Nala Money waliweza kufafanua na kutoa majawabu ya changamoto mbalimbali muhimu za wadau. CEO Alimshukuru sana Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Bw. Kayu Ligopora kwa maandalizi mazuri ya mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa HARD ROCK Athens siku ya ijumaa tarehe 16/06/2023.
Siku ya Jumamosi tarehe 17/06/2023 ilikuwa ni siku maalum ya kukutana na ndugu wote wa Afrika Mashariki. Aidha siku hii pia aliendelea kufafanua na kutatua changamoto zote muhimu.