2 0
Read Time:7 Minute, 35 Second

Na Mwandishi wetu

WU® MEDIA

Hotuba ya Balozi Kairuki kwa Diaspora China

Balozi Kairuki akiongea na Diaspora katika hafla ya kuagwa iliyoandaliwa na Diaspora wa Tanzania nchini China.
Ndugu Khatib Makenga, Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania Guangzhou

Ndugu Ahmed Saleh Tamin; Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini China;
Dkt. Tausi Kida, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji,
Ndugu Khatib Makenga, Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania Guangzhou;
Wanadiaspora wote mliopo hapa jioni ya leo;
Wageni Waalikwa; Mabibi na Mabwana;

Ninawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kwanza naomba niaze kwa kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehemu aliyetujaalia kuifikia siku ya leo na kutuwezesha kujumuika pamoja hapa Guangzhou jioni hii.

Pili naomba kutoa Shukrani zangu za dhati kwa Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Guangzhou chini ya Uongozi wa Ndugu Ahmed Saleh Tamin pamoja na Ofisi ya Konseli Mkuu ya Tanzania jijini Guangzhou chini ya Uongozi wa Ndugu Khatib Makenga kwa kuandaa hafla
hii ya kuagana.

Aidha, ninamshukuru kiongozi wetu- Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Dkt. Tausi Kida na ujumbe wake unaomjumuisha Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC ndugu Gileard Teri kwa kujumuka nasi siku ya leo.

Ndugu Wanadiaspora,
Risala yenu imesema mengi.

  • Hivyo,sipendi kuwachosha zaidi na maneno mengi.
  • Zaidi Nami nitumie fursa hii kuwashukuru sana nyote kwa ushirikiano mkubwa mlionipatia katika kipindi chote nilichohudumu kama Balozi wa Tanzania hapa China kwa miaka 6.
  • Kwa hakika bila ushirikiano wenu isingekuwa rahisi kupata mafanikio yaliyopatikana. Lakini nikiri wazi kwamba, KWELI TUMEVUNA manufaa mengi, LAKINI NI KWELI PIA KWAMBA hatujavuna kiasi cha kutosha.
  • China ina fursa nyingi sana…..THE SKY IS THE LIMIT kwa fursa.
  • Hivyo, nitoe rai kwa wanadiaspora na watanzania wote msisite wala kuona aibu kuchangamkia zaidi fursa za kiuchumi na kijamii zilizopo CHINA.
  • Mama Samia katika ziara aliyoifanya hapa CHINA mwezi NOVEMBA mwaka jana amefungua zaidi njia yenye FURSA lukuki. Kazi kwetu TUJIPANGE, TUZICHANGAMKIE.
  • NinawasihitutumieushirikianowetunaChinailikupata mbinu za kuongeza tija katika uzalishaji kule nyumbani iwe ni kwenye kilimo, au Madini, au Uvuvi au Mifugo. Tujiwekee dhamira ya kuachana na kuuza bidhaa ghafi ndani ya miaka 10 ijayo.
  • Kwa Wanafunzi- msiache kutumia fursa ya kusoma China kupata ujuzi utakaowawezesha kusaidia nchi yetu kutumia rasilimali zake.
  • Na hapa niweke msisitizo- mkiweza pendeleeni kusoma KOZI zinazofundishwa kwa lugha ya Kichina ambazo Wachina wenyewe wanasoma.
  • Hizi programu za zinazofundishwa kwa lugha kiingereza hazifikii viwango vya juu kama zile za Kichina. Kwa kufanya hivyo, mtapata elimu BORA.

Na humo humo pia mtapata marafiki wa kichina ambao mnqwesa kushirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali baada ya kumaliza masomo yenu.

Wafanyabiashara msiache kuchangamkia fursa za china za kupata teknolojia za kusaidia kuongeza thamani ya Bidhaa mbalimbali ili tuachane na kuuza bidhaa ghafi.

  • Mliopo China endeleeni kufungua macho kujifunza teknolojia za wenzetu za uzalishaji wa bidhaa ambazo zinazalishwa hapa China kwa kutumia malighafi zinazotoka kwetu.
  • kama wachina wananunua kilo moja ya tumbaku kwa DOLA 1, alafu wanaitumia tumbaku hiyo kuzalisha sigara za thamani ya Dola 100. Maana yake wenzetu wanafaidika sana. Na mfanyabiashara anachotaka ni faida. Hatutegemei wachina watoke hapa China kwenda kujenga kiwanda cha kuzalisha sigara Tanzania wakati anaweza kununua tumbaku kwa bei chee kutoka kwetu- –na kuja kupata faida maradufu.Hivyo, lazima sisi tuamke- tufanye utafiti, tuifahamu teknolojia ya kukausha tumbaku, kuchakata tumbaku hadi kuzalisha sigara.
  • Na hapa nitoe rai kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Ofisi yetu ya Konseli Kuu Guangzhou- endeleeni na ile programu yenu nzuri ya Elimu kwa umma- kuwafungua macho watanzania wenzenu wajue fursa zilizopo.

Ndugu Zangu,

  • Kwakuwa ninaelekea kwenye KITUO KIPYA nchini
    UINGEREZA, niwahakikishieni kwamba ninakwenda kuendeleza KAZI KUBWA NA NZURI iliyofanywa na Balozi wetu aliyemaliza muda wake Mhe. Dkt. Asharose Migiro.
  • Kule ninapokwenda kuna DIASPORA ya Tanzania kama ilivyo hapa.
  • Moja ya mambo ninayotamani kufanikisha ni kuiunganisha DIAPORA iliyopo Uingereza na Diaspora ya hapa ili kuona namna gani mnaweza kushirikiana kuchangamkia fursa lukuki zilizopo hapa China kwa manufaa ya nyumbani Tanzania.
  • UCHUMI WA UINGEREZA unategemea zaidi biashara ya HUDUMA— (Service Industry). Hawazalishi bidhaa sana kama ilivyokuwa miaka ya zamani. Wanategemea zaidi kuagiza bidhaa kutoka nje. Hiyo ni fursa kwa Diaspora yetu iliyopo Uingereza na China.

Kwa kutumia mitaji midogo tu wanayoweza kuipata ama kutokana na vipato vyao au mikopo katika Mabenki ya kule, wanaweza kupata bidhaaa kutoka China kwa ajili ya kuanzisha shughuli za uzalishaji kule nyumbani…na hapo watakuwa wametoa mchango wa moja kwa moja kwa
uchumi wa nchi yetu.

Aidha, Diaspora iliyopo UK na nyinyi mliopo China mnaweza kuunganisha nguvu kuwekeza katika miradi yenye tija na faida kwa nchi yetu kwa mitaji nafuu. UMOJA NI NGUVU- hakuna cha kushindana….kuna fursa kwa kila mmoja.

Hivyo, Ndugu TAMIN na diaspora wenzio—hatuagani hapa- KAzi kati yangu na nyinyi itaendelea- japo kwa kofia nyingine. Nitashirikiana na Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar na Konseli Mkuu Makenga kufanyia kazi wazo hili.

Ndugu Zangu,

  • Tulipokutana kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba 2017 tulipanga kufanya mengi yenye tija na manufaa kwa diaspora na nchi yetu kwa ujumla kupitia mahusiano yetu na Taifa la China.

Tumefanikiwa mengi,lakini hatukuweza kuyamaliza yote kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwemo mlipuko wa UVIKO19 ambao ulipelekea miaka mitatu kupita bila kufanya mambo mengi sababu ya hatua za udhibiti zilizochukuliwa na wenyeji wetu.

  • Pamoja na changamoto hiyo na nyinginezo, ninaamini kabisa kwamba tulipo leo ni bora zaidi ya kule tulipokuwa miaka 6 iliyopita.

Hivyo ninafarijika kwamba nimetoa mchango wangu kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Sina shaka kwamba Mheshimiwa Balozi Mteule Khamis Mussa Omar na timu yake wataendeleza haya yote na kuzidi.

  • Bahati nzuri, BALOZI OMAR NI MTU ANAYEIFAHAMU VIZURI CHINA na MAHUSIANO YA NCHI YETU NA CHINA. Ni MTU MUUNGWANA, MTU RAHIMU, MCHAPAKAZI HODARI NA MTU ANAYEFIKIKA. Hana Mikogo wala Urasimu.
  • Ninawaombeni kila mmoja wetu ampe ushirikiano Mhesomiwa Balozi OMAR ili aweze kutimiza matarajio na matamanio yenu ya kuona fursa za uchumi zilizopo China.

Ndugu Zangu,

Naomba nimalizie hotuba yangu kwa kutoa shukrani.
Kwanza ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani yake kwangu. Kazi ya kumwalikisha hapa China ilikuwa nyepesi kwasababu ya miongozo na maelekezo yake thatibi.
Kwa hakika mahusiano ya nchi yetu na Taifa la China yameimarika sana katika Nyanja zote katika kipindi chake.

Ninamshukuru pia kwa kuendelea kuniamini na kunipa majukumu ya kuwakilisha nchi yetu nchini UINGEREZA. Ninamuahidi Utiifu, Uaminifu na uchakakazi hodari utakaoleta manufaa kwa nchi yetu na watu wake.

Nitakuwa mchonyo wa fadhila, nisipotambua na kutoa shukrani za dhati kwa Rais aliyetangulia Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye aliniteua kuwa Balozi katika Taifa la China. Ninamuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumpa pumziko la Milele. AMEN.

Aidha, ninatoa shukrani kwa Wasaidizi wote wa Mheshimiwa Rais kuanzia Mheshimiwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje wa sasa na waliopita na viongozi wengine wote Serikalini, Sekta

Binafsi na Taasisi mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine wana mchango mkubwa katika kufanikisha majukumu yetu.

Ndugu Zangu,

  • Pamoja na salaam za jumla kwa wadau, niruhusuni nitoe shukrani kwa wafuatao ambao kwa namna moja au nyingine wana mchango muhimu ulioniwezesha kufanikisha majukumu yangu nikiwa hapa CHINA kama Balozi.
  • Nianze kutoa shukrani zangu za dhati kwa viongozi wote wa Diaspora tulioshirikiana katika kipindi cha miaka 6- kuanzia Mwenyekiti wa kwanza niliyemkuta nilipowasili mwaka 2017 Mzee JOHN RWEHUMBIZA na timu yake ya uongozi, mwenyekiti aliyefuatia Ndugu ABRAHAM MELISHANI na timu yake na sasa Ndugu AHMED SALEH TAMIM na timu yako.
  • Ninawashukuru kwa ushirikiano wenu mkubwa, msaada wanu na ushauri wenu wa hekima na busara ambao umewezesha mafanikio tuliyoyapata katika kujenga diaspora imara hapa CHINA.
  • Ninatambua kujitolea kwenu kwa hali na mali. Wakati mwingine mmepitia misukosuko mingi, na wakati mwingine mlibebeshwa lawama zisizokuwa zenu.
  • Daima mmeonyesha ukomavu, uimara na kutotetereka – lakini ndio UONGOZI unavyokuwa.
    Sifa ni zako, na lawama pia ni zako…hauwezi kumfurahisha kila mtu kila wakati.
  • Pili, ninatoa shukrani za dhati kwa Watumishi wenzangu wote wa Ubalozi BEIJING na KONSELI KUU Guangzhou na Ofisi ya Air Tanzania hapa Guangzhou kwa msaada wenu, ushauri wanu na ushirikiano wa karibu mlionipatia katika kipindi hiki cha miaka 6.
  • Mini nilikuwa uso wa Ubalozi (Face of the Embassy) lakini nyinyi mlikuwa WAWEZESHAJI wa yote tuliyofanya (UNSUNG HEROES). Kwa kweli mafanikio haya tunayozungumza leo yameletwa na juhudi zenu.
  • Ninawatakia kila la heri katika kuendeleza kusukuma gurudumu la uwakilishi hapa CHINA.
  • Tatu, naishukuru sana familia yangu. Namshukuru mke wangu Mheshimiwa. Angellah Kairuki kwa mchango wake mkubwa ulionipa utulivu wa kutekeleza majukumu yangu. Upo msemo kwamba, kwa kila mwanaume mwenye mafanikio, yuko mwanamke, nawaambia ni kweli. Angellah has been and continues to be my dependable support system.

Shukrani zangu pia,ziendee wanangu na Ndugu Zangu WOTE kwa kunivumilia katika kipindi chote cha miaka 6 nilipokuwa hapa CHINA kwa kwa sala na dua zao wakati wote. Ahsateni sana.

  • Na Mwisho lakini sio mwisho wa umuhimu ninatoa shukrani zangu za dhati kwenu nyote Watanzania wenzangu mliopo hapa Guangzhou, na wale mliopo katika Majimbo mengine yote ndani ya Jamhuri ya Watu wa China.
  • Ninawashukuru kwa ushirikiano mkubwa mlionipa wakati wote nikiwa Balozi hapa China. Nitawa-miss kama mtumishi, Kaka, Rafiki na kiongozi wenu.
  • Tuendelee kuombeana dua njema ili tuweze kutimiza wajibu wa kutumikia watanzania wenzetu kila mmoja kwa nafasi yake na karama yake.
    Asanteni kwa kunisikiliza!

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %