0 0
Read Time:1 Minute, 46 Second

Milano, Italia

Waziri Mkuu awahamasisha Wataliani kuwekeza Tanzania na kutembelea vivutio vya UTALII

Ataja msimamo wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia wa kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini

Milan 2023

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa nchini Italia kuja Tanzania kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kuwa Tanzania ina malighafi za kutosha pamoja na uwepo wa masoko ya uhakika kutokana na eneo la kijiografia.

“Msisitizo wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mkakati wa Serikali ni kuwahamasisha wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa mbalimbali nchini waje kuwekeza katika ujenzi na kuzalisha bidhaa hizo nchini ili zipatikane kwa wingi na kwa urahisi.”

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 19, 2023) wakati akizungumza katika Jukwaa la Tatu la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Italia lilifanyika Palazzo Regione Lombardia, Milan nchini Italia. Waziri Mkuu yuko nchini Italia akimuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 hadi Oktoba 20, 2023, Rome nchini Italia.

Mheshimiwa Majaliwa ametaja baadhi ya maeneo ambayo wawekezaji hao wanaweza kuja kuwekeza katika sekta za madini, kilimo, mawasiliano, mifugo, uvuvi, utalii na afya hivyo amewakaribisha wafanyabiashara hao na wawekezaji watumie fursa hiyo na kuwekeza nchini.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa sasa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara, viwanja vya ndege na nishati ya uhakika ili kurahisisha shughuli mbalimbali zikiwemo za uwekezaji.

Taasisi hizo ni pamoja Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Kukuza ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) ambao viongozi wake walipata fursa ya kutaja fursa za uwekezaji zilizopo nchini pamoja na namna ya kuwawezesha kuyafikia maeneo hayo.

Milan 2023
Waziri mkuu akiongea na wadau mbalimbali kwenye Kongamano la biashara lililoanza Leo tarehe 19/10/2023 jijini Milan Italy.
Balozi wa Tanzania nchini Italy Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiongea katika ufunguzi wa KONGAMANO la tatu la biashara na uwekezaji, kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Waziri mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa aliye muwakilisha Mh RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan.
DIASPORA
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %