0 0
Read Time:38 Second

WORLD TRAVEL MARKET (WTM)

Tanzania yatumia maonesho makubwa ya utalii duniani ya WTM kuwaleta watalii Tanzania

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kuhakikisha kuwa inatimiza malengo iliyojiwekea kama nchi ya kupata watalii milioni tano na kuliingizia taifa zaidi ya dola za kimarekani bilioni sita kwa mwaka, hivi sasa inashiriki maonesho makubwa ya utalii duniani ya World Travel Market (WTM) yanayoendelea nchini Uingereza ili kutangaza urithi na hazina kubwa ya vivutio vya utalii ambavyo vinapatikana Tanzania.

Akizungumza jijini London kuhusu mafanikio ya ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya WTM ya mwaka huu, kiongozi anayeongoza ujumbe wa TTB katika maonesho hayo Mtendaji Mkuu wa TTB Ndugu Mfugale amesema tayari wameshafanya majadiliano na kushawishi makampuni kadhaa makubwa duniani kuwaleta watalii nchini mapema mwakani.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %