
WU® MEDIA
Na YUSUFU ALLY MGENI
TAARIFA ZA KIKAO CHA BALOZI NA VIONGOZI NA WAJUMBE
Taarifa ya Maazimio ya Kikao:

(1) Vitambulisho na haki za watanzania waishio nje ya nchi
Serikali inatambua kua kuna watanzania wengi waishio nje ya nchi wakiwa hawana vibali
(A) labda wamepoteza paspot
(B) au hawana kabisa
(C) au wamejiripua kwa kutumia vitambulisho vya nchi zingine ili kutafuta namna yakuishi ktk nchi hizo walipo
Hivyo Muheshimiwa Raisi Mama Samia suluhu ameamua kuanzisha kitambulisho Maalum kitakacho kutambulisha kama mtanzania Diaspora unae ishi nje ya Tanzania hata kama unaishi nje ya nchi kwa kutumia kitambulisho cha taifa lingine
Hivyo kadi hiyo itakupa hadhi Sawa na Raia wengine nchini
Wale wasio kua na vitambulisho ubalozi umewashauri kujiorodhesha ili kuweza kuwapatia passport kwa njia zakisheria kwa online applications

2 MASWALA YA KUSAFIRISHA MAITI
SERIKALI IMEAMUA KUITUMIA BANK YA CRDB NA KUWEKA KIPENGELE MUHIMU CHA KUGHRAMIA GHARAMA ZA KUSAFIRISHA MAITI NA KUTOA MKONO WA POLE WA KIASI CHA SHILINGI MILIONI TANO KAMA MKONO WA POLE
(A) balozi watawaalika bank ya CRDB kuja kukutana na watanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo ya ki bank
(B) ukiwa na account ya CRDB utaweza KUWEKA pesa yako hiyo ktk account kidogo kidogo kwa maana yakujiwekea akiba
Kuna unapata pesa nyingi na huwezi Kusafiri nazo kwa mujibu wa sheria za airport unaweza uzidumbukiza ktk account na ukazikuta nyumbani
Ubalozi umewataka watanzania kuendelea kuwekeza nyumbani
Hata ile R 100 unayotuma nyumbani ni mchango pia maana miamala inakatwa kodi
Hivyo kwa Takwimu za Serikali ktk budjet ya MWAKA huu Diaspora wameweza kuagiza pesa nchini KIASI cha Dollar za kimarekani Bilioni moja nukta mbili
Hivyo utaona umuhimu wako kua nje ya nchi
Ubalozi umewataka viongozi kua na takwimu ya watanzania ktk kila jimbo ili kua Rahisi ktk kushughulikia matatizo ya watanzania tuishio south africa
Hivyo uongozi utaanda form Maalum itakayo pita kila maskani kwa ajili ya kujisajili ili tuweze kua na idadi kamili
Uongozi wako wa kwa zulu Natalie unakuomba ushirikiano huo ili kufikia lengo hilo
