WU® MEDIA
O.J. Simpson(1947-2024)
NYOTA WA ZAMANI WA NFL NCHINI MAREKANI
Mwanasoka wa zamani nchini Marekani, OJ Simpson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76. Familia yake imesema OJ amefriki dunia kutokana na saratani siku ya Jumatano na wakati akiaga dunia alizungukwa na watoto na wajukuu zake.
Nyota huyo mweusi wa NFL alikuwa miongoni mwa wachezaji wakubwa wa kizazi chake. Mnamo mwaka 1994, alishtakiwa kwa mauaji ya mkewe Nicole Brown na rafikiye. Kesi yake kwenye televisheni ikawa moja ya wasifu wa juu zaidi wa karne iliyopita – ikionyesha mgawanyiko wa rangi nchini Merika.
Simpson aliachiliwa lakini baadaye akapatikana na hatia ya mauaji katika kesi ya madai. Kando na maisha yake ya soka, OJ Simpson pia alijishughulisha na uigizaji akionekana katika utayarishaji na filamu nyingi za televisheni ikiwa ni pamoja na mfululizo wa kibao cha “The Naked Gun”.
Mnamo 2007, Simpson alihukumiwa kwa wizi wa kutumia silaha katika kesi tofauti na alitumikia kifungo cha miaka tisa jela.