TANZANIA
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi. Mahmoud Thabit Kombo ameandika katika ukurasa wake binafsi wa Instragram maneno ya masikitiko kwa msiba wa ghafla wa Dkt. Ndungulile.
Dkt. Faustine Ndungulile aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, alishinda kwa kishindo na kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa WHO wa Afrika na alitakiwa kuanza kazi rasmi katika nafasi hiyo mwezi februari mwakani 2025
Mipango ya kuurejesha mwili wa marehemu kutoka india ambako alifariki wakati akipatiwa matibabu inafanywa,nae spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema taarifa na taratibu za mazishi zitatangazwa.