0 0
Read Time:1 Minute, 37 Second

WU®MEDIA

  • Waziri Kombo apongeza mageuzi ya uchumi na utulivu wa kisiasa unaoendelea nchini humo
  • Wautaja umoja amani na usalama wa Tanzania kuwa ni mfano wa kuigwa Afrika

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia zimesaini hati nne za makubaliano ya ushirikiano katika mkutano uliofanyika jijini Mogadishu leo tarehe 19 Disemba 2024 chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Ahmed Moalim Fiqi.

Hati hizo nne zilizosainiwa zimehusisha Ushirikiano wa jumla, sekta ya Utalii, Ulinzi na Afya. Hatua hiyo inalenga kukuza ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi sambamba na kuboresha utoaji huduma kwenye sekta hizo kwa manufaa ya raia wa mataifa yote mawili.

Waziri Kombo akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa hati hizo Waziri Kombo ameeleza Tanzania imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma za afya ambapo kupitia makubaliano hayo Somalia watapata fursa ya kunufaika na huduma mbalimbali zinazopatikana nchini kwenye sekta hiyo ikiwemo matibabu, kununua madawa na vifaa tiba na mafunzo.

Aliendelea kueleza kuwa Serikali za pande zote mbili zinatambua kuwa ili wananchi waweze kunufaika na fursa hizo ni muhimu kuhakikisha huduma za mawasiliano na usafiri kati ya Tanzania na Somalia zinaimarishwa. Hivyo amehimiza kuharakishwa kwa mazungumzo yanayoendelea ili huduma ya usafiri wa moja kwa moja kwa njia ya anga kati ya Dar es Salaam na Mogadishu ianze kupatikana mapema iwezekanavyo.

Aidha Waziri Kombo ameelekeza watendaji kuandaa utaratibu maalumu wa kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa mikataba mamkubaliano yaliyofikiwa huku akihimiza kuwa nataka kuona ikitekelezwa kwa vitendo.

Ushirikiano huu utasaidia mataifa yetu kufikia malengo yake ya kiuchumi sambamba na kukidhi matarajio ya Wakuu wa Nchi zetu ambao dhamira yao nikuona ustawi wa uchumi wa wananchi kupitia fursa zainazotokana ushirikiano huu. Hivyo ni muhimu kwetu sote kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa vitendo. Alieleza Waziri Kombo.

Somalia
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %