0 0
Read Time:45 Second

Tanzania na Saudi Arabia zasaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano Katika kuendeleza Sayansi na Elimu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Aprili 13, 2025, nchini Saudi Arabia, imesaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia katika kuendeleza Sayansi Sayansi Teknolojia na Elimu.

Hati hiyo ya Makubaliano imesainiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda na Waziri wa Elimu na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya HCDP ya Saudi Arabia Mhe. Yousef bin Abdullah Al-Benyan.

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika masuala ya elimu, utafiti na sayansi.

Tukio hilo limeshuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Dkt. Moh’d Juma Abdalla, Katibu Mkuu Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia Prof.
Carolyne Nombo, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Prof. Peter Msofe na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya ufundi Stadi Dkt. Fredrick Selukele.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %