
Maandalizi ya AFCON 2027 Waziri Makonda Alimkaribisha Rio Ferdinand
DAR ES SALAAM – Katika harakati za kupanua ushawishi wa Tanzania kimataifa na kuleta fursa za kiuchumi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Micheza, Mhe. Paul Makonda, alimwalika mwanasoka maarufu wa kimataifa, Rio Ferdinand, kufanya ziara rasmi nchini Mei 2026. Hatua hiyo haikuwa tu kwa wapenzi wa michezo bali ilikuwa ni diplomasia ya uchumi na siasa kupitia michezo.
Akizungumza Mei 19, 2026 baada ya kumkaribisha mwanasoka Ferdinand kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Waziri Makonda alisema ziara hiyo ilileta ujumbe chanya kwa jamii ya kimataifa kuhusu uwezo wa Tanzania katika maandalizi ya michuano hiyo ya bara la Afrika.
Katika mahojiano yake na vyombo vya habari, Ferdinand alisema alivutiwa kuja nchini kwa sababu Tanzania ni nchi nzuri na yenye mapenzi makubwa ya soka pia, nyota huyo alieleza kuwa ziara yake ililenga kuchunguza fursa za kwa pande zote mbili katika utalii, kuvumbua vipaji vya vijana, na kubadilishana tamaduni.
“Kwangu mimi, safari hii ilihusu watu, utamaduni, soka, na fursa. Tanzania ina shauku kubwa ya michezo na kizazi kipya chenye nia kufanya vizuri katika soka , Nilitarajia kujifunza zaidi, kukutana na watu ana kwa ana, na kuona jinsi tunavyoweza kujenga fursa za pamoja katika siku zijazo,” alisema Ferdinand.
Pia alishukuru kwa nafasi ya kukutana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa kitaifa, akisema: “Ilikuwa heshima kubwa kupata nafasi hii ya kukutana na Mhe. Rais na viongozi wengine wakati wa ziara yangu, na nilitazamia kujifunza zaidi kuhusu nchi hii nzuri.”
Kwa upande wa faida za kidiplomasia ya uchumi, Tanzania ilipata kichocheo cha kuvutia wawekezaji kutoka Ulaya na nchi nyingine. Ferdinand, akiwa balozi wa utalii na uwekezazi wa Tanzania, aliahidi kuitumia jina lake kimataifa kuvutia wageni na mitaji. Aidha, serikali ilichukua nafasi ya mkakati huo kuonyesha ukomavu wa kisiasa, amani, na mazingira rafiki ya uwekezaji. Ushirikiano huo uliimarisha pia hadhi ya Tanzania katika maandalizi ya kushiriki kwa nchi hiyo katika mashindano ya AFCON 2027.








